





Huduma yaReli ya KATI IENDAYO mikoa Tabora, Kigoma na Mwanza
imerejea tena leo hii baada ya kusimamishwa kwa takribani mwaka na ushee tokana na sababu mbalimbali na lililokuwa shirika la reli nchini au TRC.
Huduma hii inarejeshwa tena na mmiliki mpya toka India TRL ambaye amekabidhiwa shirika hili takribani mwezi tu uliopita, moja ya sababu ya kushindwa kwa TRC ilikuwa ni uchakavu na uchache wa mabehewa na ingini, mwezi tu baada ya kukabidhiwa safari zaruia upya, hatujasikia ujio wowote wa ingini wala mabehewa mapya lakini safari zarejeshwa ambapo zitakuwa mara mbili kwa wiki.
Je kama TRC walishindwa kwa sababu hizo hapo juu, hawa wawekezaji toka India kwa kutumia mabehewa na ingini zilezile warejesha trip hizi kunani hapa?
je haya mabehewa amabayo mengine yafanyiwa matengenozo dakika kabla ya safari yatamudu? kuna ukarabati wowote hapa?
angalia behewa la daraja la tatu, jamani karne hii ya 21 bado twatumia mabehewa ya machuma haya kwa safari ya siku tatu?
Hii ni sawa?
Ku wapi kwenda kwetu na wakati?
1 comment:
JOMBAA SHUKRANI KWA PICHAA ZA MATUKIO MBALIMBALI. HONGERA PIA KWA KUKAMATA JIKO...
SASA NAOMBA TUWEKEE PICHA ZA VIGOGO KWENYE MKUTANO MKUU WA CCM DODOMA HVILEO
Post a Comment