Pages

March 25, 2015

SHIBE INAPOUA KULIKO NJAA! OBESITY KILLS MORE PEOPLE THAN HUNGER

Shibe inapoua kuliko njaa   Obesity kills more people than hunger
Most of the world's populations live in countries where overweight and obesity kills more people than underweight. WHO

Ukame mkali ulisababisha njaa kubwa na hatimaye wengi kupoteza maisha. 
Baadhi yetu tatakuwa tunakumbuka miaka ile 70 kuja 80 kwa Afrika na karne ya 18 na 19 kwa baadhi ya nchi duniani, watu wengi sana walipoteza maisha kwa ukosefu wa chakula bora ama utapiamlo, kama nilivyosema si wote watakuwa wanakumbuka, lakini wapo baadhi wanakumbuka.



Janga hili halikuwapata binadamu bali mpaka wanyama nao waliathirika
Vifo vya utapiamlo vimekuwepo duniani kote, mfano watu Zaidi ya milioni moja walikufa kule Ireland kati ya mwaka 1845 na 1852, wakaiita “GREAT IRISH FAMINE”  China pia walipitia kipindi kama hiki kwa miaka 3 kati 1958 – 1961, ambapo inasemekana watu Zaidi ya milioni 20 walipoteza wao walikiita kipindi “THREE YEARS OF GREAT CHINESE FAMINE” Pia tatakumbuka ukame mkali na wakutisha uliotokea pembe ya Africa na kupelekea njaa ya kutisha na vifo Zaidi ya laki moja.
Vifo hivi ni majanga ya asili tunaweza tusiwe na uwezo navyo sana Zaidi ya kutoa msaada kwa waathirika lakini dunia hivi sana inashuhudia ongezeko la la kasi vifo vinavyotokana na mtindo wa maisha, yaani watu wengi pasipo kujua wamechagua mitindo ya maisha hatarishi inayowaua taratibu kiasi kwamba si rahisi kujua.

Hii ni summary ya ripoti ya kwanza ya WHO iliyotolewa 2010


Mwaka 2008 vifo vilivyotakana na mitindo ya maisha hatarishi ilikuwa ni asilimia 63% ya vifo vyote dunia, takwimu za shirika la afya duniani zinaonyesha kuwa kati ya million 57 duniani kote vifo milioni 36 vilitokanana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ama ya mitindo ya maisha.
WHO wanasema,   “Noncommunicable diseases (NCDs), such as heart disease, stroke, cancer, chronic respiratory diseases and diabetes, are the leading cause of mortality in the world”.
 




Hii ni ripoti ya pili iliyotoka mwaka 2014, ripoti zote hizi waweza kuzipata na kuzidownload katika website ya WHO.
Ripoti ya sasa 2014 ya WHO inaonyesha kasi ya kutisha ya vifo hivi, wakati duniani kwa ujumla vifo vimepungua  kwa takribani milioni moja lakini vifo vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza vimeongezeka kwa milioni Zaidi, kutoka milioni 36 (2008) mpaka milioni 38 (2014) hii ni sawa na ongezeko la asilimia tano, kutoka 63% - 68%.


Je makadirio yakoje? Haya ndio yanaogopesha Zaidi hasa kwa bara letu la Afrika, naomba ninukuu sehemu ya ripoti ya WHO, “NCD deaths are projected to increase by 15% globally between 2010 and 2020. The greatest increases will be in the WHO regions of Africa, South-East Asia and the Eastern Mediterranean, where they will increase by over 20%. In contrast, in the European Region, WHO estimates there will be no increase. In the African Region, NCDs will cause around 3.9 million deaths by 2020”. WHO GLOBAL STATUS REPORT ON NONCOMMUNICABLE DISEASES 2014
 


Ulimwengu wa Digitali umekuja na janga lingine, Kingamuzi, vingi vina chanel sana mpaka 700 nyingi ni miziki na muvi mtu aweza kukaa hata wiki nzima hajatembea hata kilomita 2, yuko kwenye kochi na rimoti anabadilisha chanel tu.
Nilipoisoma ripoti kwanza sukuielewa, au niwe mkweli sikutakata kukubali ukweli huu, kwamba Afrika kutakuwa na ongezeko kubwa mpaka asilimia 20 alafu Ulaya hakutakuwa ongezeko, yaani 0%, tofauti kubwa ya sisi na Ulaya ni elimu au ufahamu, wenzetu hawachukulii mambo kirahisi, fikilia kuwa mwezi uliopita jirani kafa na presha, wiki iliyopita ndugu kafa na kansa ya colon, wiki hii kazini mmezika mfanya kazi mwenzenu kwa tatizo la ugonjwa wa moyo bado mtu anasema life as usual, kama kwamba hayamuhusu mpaka yamkute, Ulaya wameliona mapema wakachukua hatua.


 Albert Einstein  aliwai sema kuwa “once you stop learning, you start dying”  hiki ndicho kinatusibu sisi wa kizazi cha dotcom, kizazi cha fesibuku, twita, insta …laiti tungelikuwa tunajua kutumia karne hii ya maendeleo makubwa na ya kasi ya Sayansi na Teknolojia tungeliweza kujiuliza maswali na kusearch mtandaoni na kujua kuwa kumbe kwa mujibu wa shirika la afya duniani, tungejua kuwa kumbe vifo hivi vyaweza kuepukwa kwa maarifa ya kawaida tu,  “The NCD threat” inasema sehumu ya ripotican be overcome using existing knowledge.”
 

Huu ndio ukweli tunahitaji maarifa ya kawaida tu yanayotuzunguka ili kuepukana na vifo hivi, bahati moja mbaya kwa vijana wengi wakishamaliza chuo unakuwa kama ndio mwisho wa kujifunza, walikuwa wakisomea mitihani, wanaposikia elimu au semina za afya wanaona haziwahusu, kwa sababu ana elimu nzuri, anafanya kazi Vodacom, airtel au serikalini nk, hawajui kuwa kinachowafanya waonekane wa thamani ktk mashirika, makampuni au serikalini walipo ni hiyo afya wanayodhani wanayo, na wanayoendelea kuibomoa kila uchao. kadiri kipato kiongezekavyo ndivyo madhara makubwa Zaidi yanavyotokea katika afya badala ya kuwa kinyume chake.

Magonjwa haya yako katika makundi mawili, moja ni BIG FOUR na Mengine ni yale yasiyopewa kipaumbele.
Ripoti ya mwaka 2008 inaonyesha kuwa vifo vya mapema ama watu ambao hawajafikisha umri wa miaka 60 vilikuwa sawa na asilimia 29% , ripoti ya sasa inaonyesha ongezeko kubwa, kutoka 29% mpaka 48%, kwa kasi kizazi cha sasa kufikisha miaka 50 ni ndoto, labda uamue kuchukua hatua sasa hivi, itafute hii elimu popote pale inapopatikana, kwa bahati njema elimu hutolewa bila kiingilio chochote, lakini ndio madara yenye maudhurio hafifu.

Dr. Otto H. Warburg alifanya utafiti uliompatia tuzo ya Nobel, ambapo aligundua kuwa kila mtu awaye yoyote mwenye kansa ana tindikali nyingi mwilini, “Every single person”, inasema sehemu ya utafiti wa  Dr Otto Warburg, “who has cancer has a PH that is too ACIDIC”, watu wanaenda hospitali wanaambiwa asidi imezidi mwilini, wala hawawi wadadisi, wala hawahoji hii ina maana gani kwa afya zao, na huyo Dk. mwenye nafasi kukujibu maswali yako kama yuko waweza kumpata kwa baadhi ya hospitali binafsi, tena kwa gharama nyingine, lakini kwa hospitali zetu za umma hilo ni kama kuokota dhahabu mchangani.


Wingi wa Asidi hudhoofisha mfumo mzima wa kinga mwilini hii, utengeneza mazingira rafiki kwa matatizo mengi ya kiafya yakiwamo Uzito kupita kiasi, Presha za kupanda na kushuka, ongezeko la Cholesterol, Inni na figo kushindwa kufanya kazi sawasawa, kisukali, magonjwa ya moyo, cancer,  kupooza nk.  Na asidi nyingi mwilini usababishwa na kula kwa wingi sana vyakula vyenye asidi


Graphics kwa hisani ya Quick Meme
Prof. Ragnar Berg, Mwanalishe wa Kiswedish katika tafiti yake kuhusu mlo kamili na wenye afya uweje, alisema, “Our daily diet should consist of 20% ACIDIC and 80% ALKALINE food to maintain a healthy body”   sitatafsiri hii,   Je wavijua ni vyakula vyenye Alkaline ambavyo kwa mujibu wa profesa wa lishe twapaswa tule 80%?, ni vile ambavyo wengi hawavipi kipaumbele, mfano matunda, mbogamboga, vyakula vya mizizi, hebu jiulize ni lini mara ya mwisho umekula muhugo wa kuchemsha, au viazi vya kuchemsha? Katika bajeti yako matunda yana umuhimu gani? Na mbogamboga je? Wewe mwenyewe unayo majibu.


Vijana wengi wapatapo ajira nap engine kupata mwenza jamii uanza kutazama mafanikio yake kwa kitambi, kwamba kuwa na kitambi ndio mambo safi, je wajua kunanuwa na nini katika hicho kitambi? Hiyo ni homework yako, nenda youtube usearch Intestinal characteristics and lifestyle related diseases na Dr Shinya Hiromi. Jibu utakalo pata usiwe mchoyo mshirikishe na mwenzio.   

je mlo wako kwa siku ukoje,
Ukweli ni aibu kubwa sana kwamba vijana wa dotcom, Information Age wengine wana IPAD mpaka tatu, alafu unakufa kwa vifo vinavyoepukika, hizo Ipad zako wazitumiaje, smart phone zinakazi gani? ni fesibuk, twita, wasap tu? unahitaji mindset maintenance,  


Elimu hii inapatikana hapa nchini pasipo malipo yoyote, iwe kwenye maeneo ya kazi, maofisini, mashuleni au vikindi mbalimbali tutakuja na kutoa elimu, darasa hili laweza kuchukua dk 45, uzoefu unaonyesha watu wanakuwa na maswali mengi sana ni kama vile elimu mpya kwao, hii ndio yanaweza kuchukua muda wa ziada.


Hata sasa nikali na mengi ya kusema, kwani hili ni tone tu, Mungu akinipa uhai nitaanza kuchambua hathari za kila tatizo na mbinu za kuepukana nalo.
 Kwa wale mnaonifahamu au msionifahamu, msinishangae kwamba huyu jamaa sio haya mambo anayajuaje, jamani ni kale katabia kangu kabaya ka kupenda kudadisi, kutafititafiti na kusoma, ukweli nimegundua mambo mengi sana, tukijaariwa uhai na Mwenyezi Mungu mtayasoma hapa.




Mashirika na mitandao mingine yasemaje

Safe food
Obesity is now killing more people than hunger

Research results compiled from the work of nearly 500 researchers in 50 countries conclude that obesity and the diseases that arise as a result are overtaking problems related to hunger on a global scale. The Global Burden of Disease Study 2010, published in The Lancet, provides data about worldwide health trends between 1990 and 2010 and says that obesity-related deaths are occurring three times more than fatalities related to malnutrition and starvation. The report found that one in four deaths in 2010 were attributable to heart disease or stroke and 1.3 million deaths were due to diabetes. Blood pressure was found to be the biggest global risk factor for disease, followed by tobacco, alcohol, and poor diet. 

The times ya UK
Obesity kills more than hunger in march of “progress

Obesity has become a bigger threat to global healthy than child hunger, accordingMore than three million deaths in 2010 were attributed to excess body weight, three times the death due to malnutrition.

Wasiliana nami kwa namba +255 784 475576 au email:brwebangira@gmail.com


Picha na graphic kwa hisani ya WHO na mitandao mbalimbali

No comments:

Post a Comment