Pages

September 1, 2014

NGUVU YA UNABII - VIDONDA VYATOWEKA GHAFLA.



Hakika unabii unapotolewa na ufumbuzi unakuwa umepatikana, ndivyo ilivyokuwa pale vidonda vya tumbo vilipopona ghafla kwa kupitia neno la kinabii toka kwa Mtu wa Mungu Nabii BG Malisa.




Kupitia huduma ya kinabii watu wengi wamefunguliwa, waliokuwa wamepooza wametembea tena, waliokuwa na uziwi wakasikia tena, matatizo ya macho yakaisha na aliyekuwa na vidonda vya tumbo.




Katika siku ya kwanza ya semina ya siku 8 za kuvunja maagano Mtu wa Mungu Nabii BG Malisa katikati ya ibada alitoa unabii juu ya jina Esther na kuwa amekuwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo, alitoka dada mmoja na kukiri kuwa anaitwa Esther na kuwa amekuwa tatizo la vidonda vya tumbo kwa muda wa miaka sita sasa.




Mara baada ya unabii huu, Esther alipona papohapo na kuja kuthibitisha uponyaji wake mbele ya kanisa kwa kunywa soda ya coca, anasema hapo kabla asingeweza kunywa soda ya cocacola au yoyote ya gesi kwa muda wa miaka saba, alikatazwa na madaktari, na iwapo angekunywa, angeumwa sana tumbo na kutapika.



 Kesho yake Esther alirudi akiwa mwenye furaha baada ya kwenda hospitali kupima na kuambiwa kuwa hakuwa tena na tatizo la vidonda na kushuhudia kuwa tumbo halijamuuma kabisa.











Kwa shuhuda, ishara, maajabu na miujiza tembelea
www.facebook.com/ukombozichurch
www.youtube.com/saayaukombozi211

No comments:

Post a Comment