Pages

February 8, 2013

R.I.P Bishop Thomas Laiser, R.I.P Amadeus Msarikie

Bishop Thomas Laiser
Askofu Thomas Laizer wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini dayosisi ya kaskazini kati, amefariki dunia katika hospitali ya rufaa ya Seliani iliyopo jijini Arusha ambako alikuwa amelazwa kwa siku kadhaa akipata matibabu. Taarifa zaidi juu ya kifo chake tutakupatia pindi zitakapo tufikia katika dawati letu la GK.

Wakati huohuo aliyekuwa askofu wa jimbo la moshi kanisa katoliki Amedeus Msarikie amefariki dunia jana alfajiri mkoani Kilimanjaro. Askofu Msarikie alistaafu baada ya kutumika kwa muda mrefu na kuleta maendeleo mbalimbali katika jimbo la Moshi ikiwemo ujenzi wa shule pamoja na masuala ya kiroho. 

Habari kwa mujibu wa Gospel Kitaa

No comments:

Post a Comment