Pages

February 8, 2013

Mv Victoria Chupu chupu kuteketea kwa moto



Meli ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini(MSC)imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo wakichomelea sehemu mojawapo ya Meli hiyo.

Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kufurika katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini majira ya saa 8 na dakika kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa zlizo patikana toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo zimeleeza kuwa mafundi wa kampuni walikuwa wakichomelea katika moja ya vyumba vya chini vya Meli hiyo ndipo cheche za moto ulipoangukia katika sehemu ya kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka.

Hata hivyo moto huo ulithibitiwa na meli kuweza kuendelea na  safari zake kuelekea Bukoba kama kawaida. 

No comments:

Post a Comment