Katika kudhiirisha kauli ya Kamanda wa
Kanda Maalumu ya Kipolise Suleiman Kova, kuwa “uvumilivu sasa basi” kwa mara ya
kwanza nchini askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) wameonekana mitaani kusaidiana na jeshi la polisi katika kuimarisha
ulinzi katika mitaa ya Jiji la Dar es Salaam ambapo wafuasi wanaosemekana kuwa
ni wa Sheikh Issa Ponda, ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kwa makosa
mbalimbali, walikuwa wanaandamana kuelekea Ikulu kushinikiza kuachiwa kwake
bila masharti.
Si kawaida kwa JWTZ kuingia katika vurugu
za maandamano, lakini bila shaka “UVUMILIVU UWA UNA MWISHO”, labda huu ni
mwanzo wa enzi mpya, Muda tu ndio utaamua.
Picha kwa hisani ya Happiness Mnale