Pages

August 16, 2012

The power of Mindset change – Shell story

The power of Mindset change – Shell




.

Marcus Samuel, Muuza duka la vitu vya mapambo ya baharini (Makombe) katika Jiji la London, alipofanya uamuzi wa kutanua biashara yake nje ya Uingereza na zaidi katika bara Asia mwaka 1833, hakuwa akijua kuwa alikuwa anaenda kukutana na kuanzisha biashara kubwa zaidi duniani, ya Mafuta na nishati.

Katika moja ya safari zake Japan na Urusi akipeleka makombe ya baharini au Shells alikutana na biashara nyingine tofauti na aliyozoea kuifanya ya makombe, bila shaka ilimchikua muda kidogo kuamua kuingia katika biashara hii mpya, nap engine ilimgharimu sana ikiwa ni pamoja na kutafuta wataalamu, lakini zaidi gharama za kufanya biashara hii mpya kabisa kwake.

“It was during a trip to Japan that Marcus became interested in the oil exporting business then based in Baku, Russia. The Rothschilds had invested heavily in the 1880s in rail and tunnels to overcome the transport difficulties of getting oil from this landlocked base to the Black Sea and from there to overseas markets. Shipping still posed a problem as the oil was carried in barrels, which could leak and took up much space in the ship’s hold.” Shell websites

Aligundua kuna biashara nzuri sana ya mafuta iwapo ataweza kuisafirisha mpaka Uingereza au Marekani, lakini changamoto kadhaa alikutana nazo, baadhi yake ni:
Jinsi gani ya kuyatoa mafuta hayo kutoka Baku, Urusi na kuyafikisha katika Bahari Nyeusi ili yaweze kupakiwa katika meli
  • Meli za kusafirishia mafuta hayo.
  • Magari
  • Mabehewa maaalumu
  • Mapipa ya kupakia mafuta hayo, na haya yalikuwa na uwezekano wa kuvuja hivyo kupata hasara ilikuwa ni rahisi pia. Nk
Kwa changamoto hizo ilikuwa ni rahisi sana Marcus Samuel aachane na biashara hiyo na kuendelea na ile aliyoizoea ya makombe, kwani si ni tayari alikuwa anaingiza pesa nzuri tu, angeweza kuridhika na maisha yangeendelea bila shaka, lakini yasingelikuwa haya tuyajuayo leo, asingelikuwa na kitu cha kukaa na kuzungumza juu yake.

Uamuzi wake wa kubadili mtazamo na kuamua kunigia gharama na bila shaka hasara mara kadhaa, kabla ya kupata mafanikio, kuanzisha kampuni kubwa ya mafuta inayozidi kufanya vyema duniani kwa karne na karne sasa, SHELL OIL Co Ltd, ndiyo vinamtenganisha na watu wengine wa wakati wake, na bila shaka wauza duka wengine kama yeye, hatuwezi kuwasikia hao, wamesahaulika kama hawakuwai kuwapo kwa sababu hawkufanya jambo lolote la kukumbukukwa ama kuacha alama au LEGACY. Hivi leo vituo vyote vya mafuta hapa Bongo vyaitwa Shell, lakini si wengi wanajua ni kwanini.

Fursa hizi zingalipoa hata leo hii, lakini wengi wetu twafungwa na mapokeo na labda elimu zetu au uvivu na woga wa kujaribu jambo jipya, tena ambalo hatukufundishwa mashuleni au vyuoni ama hakuna aliyewai kufanya kabla, pengine hata imani potofu toka kwa baadhi ya manabii wa uongo.

Tunaoishi nyakati hizi tuna bahati sana, tunauwezo wa kutafiti juu ya biashara, kazi, fursa ama elimu yoyote kupata ukweli ama uwongo wake tukiwa majumbani mwetu, tusipokuwa wavivu, hivi sasa waweza kufanya biashara na yeyote duniani, Kuuza na kununua, kuagiza chochote na kulipa kwa kutumia vidole vyako pasipo kutoka nyumbani kwa na ukapata bidhaa ama huduma uliyoagiza ama kulipwa papo hapo ulipo.

Tukibadili mitazamo yetu twaweza kufanya chochote na kufanikiwa katika kiwango cha kushangaza, waweza usiamini kuwa ni wewe, Tuweke bidiii kutafuta ukweli wa jambo lolote kabla ya kusema hii haiwezekani au siwezi, amini kila kitu kina wezekana, Biblia, maandiko matakatifu yatuasa “JARIBU MAMBO YOTE, LAKINI SHIKENI LILILO JEMA” 1 Wathesalonike 5:21, (Prove all things, hold fast that which is good”) Isitoshe neno USIOGOPE, wataalumu wa maandiko wanasema liko mara 365, ina maana Mungu anataka kila siku iitwapo leo uwe na moyo wa ujasiri na kujiamini katika kutenda na si woga, kwani woga ni dhambi mbele za Mungu.

SET YOUR GOALS, SET YOUR DREAMS
Wasiliana nami kwa simu 0784475576 au email brwebangira@gmail.com