Pages

November 4, 2011

Watano wauawa Mwanza



Siku moja baada ya jiji la Mwanza kulindima na kuanikizwa na milio ya mabomu ya kutoa machozi katika juhudi za polisi kutawanya maandamano haramu na vurugu zilizokuwa zikifanya mahakamani na kundi la waislamu, leo tena mida ya saa tatu na nne ilikuwa kimuhemuhe, maenoe ya barabara ya Nyerere karibu na Benki ya Stanbic pale majambazi yalipovamia duka la vifaa vya ujenzi. 

Safari hii si mabomu ya machozi, la hasha ni siraha za moto zilizogharimu damu ya ya kutosha imemwagika dukani hapo majambazi matano yameteketea, jambo la kushngaza ni kuwa duka hilo liko karibu kabisa na kituo cha polisi cha pamba, yaani limetenganishwa  na barabara na kituo hicho cha mafuta. 

Je jamaa walidhani polisi wamelala au hakuna polisi kituoni? au pengine waliamua kujitoa mhanga kama Wapalestina? au siku zao zilikuwa zimefika? sijui, ila haiingii akilini.    

No comments:

Post a Comment