Pages

November 25, 2011

GAMBA LAWA LA KOBE!


Nipashe: LOWASSA AJIELEZA NEC
Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemaliza kikao chake jana huku aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, akisimama na kutoa dukuduku lake kuhusiana na tuhuma za ufisadi dhidi yake.

Kikao hicho cha siku mbili kilichoketi chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete, ambacho kilimalizika jana saa 11:30 jioni, mtoa habari wetu alikuwa ndani ya kikao hicho alisema Lowassa, alisimama na kueleza masikitiko yake juu dhana ya kujivua gamba ilivyoendeshwa wakati kikao hicho kikijadili hali ya siasa nchini.
Chanzo chetu kilimkariri Lowassa akisema kama ni suala la kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond, alitaka kuuvunja mkataba kati ya kampuni hiyo na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) mapema, lakini Rais Kikwete aliyekuwa nje ya nchi alikataa kufanya hivyo na badala yake alimwambia kuwa anasubiri ushauri wa makatibu wakuu wa wizara.

Alisema aliamua kujiuzulu nafasi zake katika serikali ili kulinda heshima ya serikali na chama chake, lakini anashangazwa na hatua ya wanaCCM wenzake na si wapinzani kuzunguka mikoani kumchafua wakidai kuwa yeye ni fisadi.

Lowassa alimkumbusha Mwenyekiti kuwa kumekuwa na utamaduni wa kupikiana majungu ndani ya chama na kukumbushia tukio la yeye (Kikwete) kuzushiwa mengi na Daud Mwakawago wakati wa harakati za kuusaka urais kabla ya 2005.

“Mwenyekiti wewe unakumbuka wakati Mwakawago alipokuja na rundo la tuhuma za hisia, isingekuwa busara za Rais Mkapa (Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa), wewe usingekuwa hapo ulipo,” chanzo hicho kilimkariri Lowassa akisema.




Daily News: NO EXPULSIONS NEC WINDS UP MEETING 
THE National Executive Committee of the Ruling Party, Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM), on Thursday ended its two-day meeting without expelling or stripping some prominent cadres of their posts as speculated earlier.

However, the Dar es Salaam Regional Party Secretary, Kilumbe Ng'enda, was relieved of his duties.

The party's Ideology and Publicity Secretary, Mr Nape Nnauye, promised reporters here on Thursday that he would address a press conference on Friday.

Sources from the meeting however told the 'Daily News' that the meeting resolved to forward the 'cleansing and skin shedding' business to the Ethics and Security Committee, and the Central Committee (CC-CCM).

"The meeting decided that any CCM member who has evidence of wrong-doing by the cadres should submit it to the two committees for appropriate action," revealed the source.

Another high-profile NEC member said the meeting resolved to 'cleanse' the party without breaking it up.

"NEC members debated the philosophy, it was decided it should be conducted with sobriety and with evidences," revealed another NEC member.




 Mwananchi: LOWASSA, SUMAYE WABWATUKA NEC
MAWAZIRI Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, jana walishambulia kwa maneno makali wajumbe wawili wa Sekretarieti ya CCM kwamba wamekuwa wakikivuruga chama na kusababisha mgawanyiko uliopo.Lowassa aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu, kutokana na kashfa ya Richmond ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumzia suala hilo wakati wa mjadala wa hali ya siasa, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichomazika jana mjini Dodoma.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zinasema Lowassa alianza kubwaga moyo wake baada ya NEC kuridhia ombi la Kamati Kuu ya chama hicho (CC) kwamba suala la mageuzi ndani ya CCM maarufu kama kujivua gamba lirejeshwe katika kamati hiyo ili lifanyiwe kazi kwa taratibu za kawaida za kinidhamu baada ya wahusika kukataa kuachia nafasi zao.

“Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,”Lowassa alinukuliwa akihoji.

Lowassa alinukuliwa akiwataja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, John Chiligati kwamba wamekuwa wakitukana watu ovyo kwa fedha wanazopewa na CCM.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Lowassa alitumia dakika saba kumshambulia Nape kwamba amekuwa akifanya mambo nje ya utaratibu na kwamba mwenendo huo umekuwa ukikibomoa chama badala ya kukijenga.

Baada ya maneno ya Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Sumaye alisimama na kuhoji sababu za chama hicho kunyamazia ukiukwaji wa taratibu ambao umekuwa ukifanywa na watendaji hao.

“Mwenyekiti huyu bwana (Lowassa) amesema kwamba amechafuliwa kwa miezi saba, sasa kama leo tunasema kwamba tunarudi kwenye utaratibu wa kamati za maadili, hao waliomchafua watafanywaje?”Sumaye alinukuliwa akihoji.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya kikao hicho zilimnukuu Kikwete akisema kwamba viongozi hao watakuchukuliwa hatua za kinidhamu kama watakuwa wamefanya hivyo.
Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwasihi wajumbe kuachana na suala hilo na badala yake kuchangia maeneo mengine ya taarifa hiyo ya hali ya siasa iliyowasilishwa na Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje ya CCM, January Makamba.

No comments:

Post a Comment