UDOM - Massive turnout for 12 posts job interview.
Hii ni UDOM na hawa ni JOB SEEKERS wameitwa kwa Interview, nafasi ni 12 tu lakini walioitwa kwa usahili ni zaidi ya 2200, Je hii yamaanisha nini hasa? pata comments za watu zaidi hapa. JAMII FORUMS
Nina uzoefu wa hali ilivyo katika ajira za kufundisha vyuo vikuu vya Marekani. Ikitokea nafasi, chuo kinawajibika kisheria kuitangaza nafasi hiyo kila mahali panapowezekana, kuanzia kwenye majarida na mitandao ya taaluma husika, na kwenye vyuo vingine. Ni lazima wasambaze taarifa sehemu hizo zote, ili kila mtu aweze kupata fursa sawa ya kuliona tangazo na kupeleka maombi.
Ni kawaida kwa nafasi hiyo moja kuletwa mamia ya maombi. Kazi sasa inakuwa kwa kamati husika kuanza kuchuja. Watachuja sana, hadi wafikie waombaji wachache, labda tuseme 20, ambao sasa kamati inawaita kwenye mahojiano.
Baada ya mahojiano hayo, wanaweza kupatikana waombaji watatu, ambao wanaitwa chuoni kufanyiwa mahojiano zaidi, na wao kuonyesha uwezo wao wa kufundisha, falsafa na fikra zao kuhusu somo husika, na kadhalika.
Baada ya hapo, anapatikana mwombaji moja, na ndiye anapelekewa taarifa ya kupewa kazi.
Nina uzoefu wa hali ilivyo katika ajira za kufundisha vyuo vikuu vya Marekani. Ikitokea nafasi, chuo kinawajibika kisheria kuitangaza nafasi hiyo kila mahali panapowezekana, kuanzia kwenye majarida na mitandao ya taaluma husika, na kwenye vyuo vingine. Ni lazima wasambaze taarifa sehemu hizo zote, ili kila mtu aweze kupata fursa sawa ya kuliona tangazo na kupeleka maombi.
ReplyDeleteNi kawaida kwa nafasi hiyo moja kuletwa mamia ya maombi. Kazi sasa inakuwa kwa kamati husika kuanza kuchuja. Watachuja sana, hadi wafikie waombaji wachache, labda tuseme 20, ambao sasa kamati inawaita kwenye mahojiano.
Baada ya mahojiano hayo, wanaweza kupatikana waombaji watatu, ambao wanaitwa chuoni kufanyiwa mahojiano zaidi, na wao kuonyesha uwezo wao wa kufundisha, falsafa na fikra zao kuhusu somo husika, na kadhalika.
Baada ya hapo, anapatikana mwombaji moja, na ndiye anapelekewa taarifa ya kupewa kazi.
Nimeeleza hayo ili tu kupanuana mawazo.