Pages

September 10, 2011

SMZ yatangaza siku 3 za maombolezo

Rais Jakaya kikwete akiwa na Rais wa SMZ Dr Ali Mohamed Shein  wakiaangalia miili ya watoto  mjini Zanzibar leo hii. 

Rais wa SMZ Dr Ali Mohamed Shein akifariji moja wa manusura wa ajali ya meli ya Mv Spice.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza siku tatu za maombolezo kufuatia ajali ya meli ya Mv Spice iliyotokea alfajiri leo ambapo watu zaidi ya 100 wanasadikika kuwa wamekufa huku 620 wakiokolewa. 

Watu wasiopungua 187 wamekufa baada ya meli iliyokuwa imezidisha mizigo kuzama katika pwani ya kisiwa cha Zanzibar ikiwa na watu takriban 800.

 Msemaji wa serikali amesema watu 620 walionusurika wameokolewa. Serikali imetangaza siku tatu za maombolezo.

 Inadhaniwa kuwa meli hiyo ilizama baada ya injini yake kukosa nguvu.
 Shughuli za uokoaji zilikwazwa kwa kuwa meli hiyo ilizama usiku.

  Meli iliyozama
 Zaidi ya watu 100 bado hawajulikani walipo, lakini watu 325 walionusurika wameokolewa, kwa mujibu wa waziri wa masuala ya dharura wa Zanzibar.

 Meli hiyo, MV Spice Islander ilikuwa ikisafiri kati ya Kisiwa kikuu cha Unguja kuelekea Pemba.

 Meli hiyo ilikuwa ikirejesha watu baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani.

 Msaada
Mamlaka za huko zimezidiwa na tukio hilo na zimeomba msaada kutoka nje.
 Serikali ya Zanzibar imeunda kituo cha uokoaji na kutoa wito kwa taasisi zote kusaidia katika shughuli za uokozi. Serikali hiyo pia imeomba msaada kutoka nchi nyingine za nje, kama vile Kenya na Afrika Kusini.

 Walionusurika walichukuliwa na boti za kibinafsi na kupelekwa katika bandari ya Zanzibar, amekaririwa kamishna wa polisi wa Zanzibar Mussa Hamis.

  Watu walionusurika wakipelekwa hospitali
 Miili ya watu imekuwa ikisukumwa katika pwani ya Zanzibar na mawimbi. Mpaka sasa miili ya watu 100 wamepatikana, amesema mwandishi wa BBC Ali Saleh akiwa Zanzibar.

 Maelfu ya ndugu na jamaa wanasubiri kusikia taarifa za ndugu zao ambao walikuwa ndani ya meli hiyo, anasema mwandishi wetu.

 Mohhamed Aboud, waziri wa masuala ya dharura wa Zanzibar anasema watu 259 walionusurika wameokolewa lakini 40 kati yao wamejeruhiwa sana.
 
kwa mujibu wa BBC.

No comments:

Post a Comment