Pages

September 8, 2011

Makombora 100 kuvurumishwa Igunga, Je ni yepi hayo???

 Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa, anasema ana makombora zaidi ya 100.



 Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, anatarajiwa kuzindua rasmi kampeni za mgombea wa CCM Jimbo la Igunga



Rais Jakaya Kikwete




....Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, atazindua kampeni za mgombea wao kesho, wakati kesho kutwa Rais mstaafu Benjamini Mkapa, akitarajiwa kuzindua kampeni za CCM na CUF itazindua kampeni zake Septemba 13.

 Akizungumza na gazeti hili, Dk. Slaa alisema wameandaa makombora zaidi ya 100 kuisambaratisha CCM na serikali yake ambayo alirejea wito wake wa mara kwa mara kuwa imeshindwa kuongoza na kusababisha maisha kuwa magumu kwa Watanzania.

 Alisema amefurahi kwamba kampeni za CCM zinafunguliwa na Mkapa kwani CHADEMA imemwandalia makombora yake ya ufisadi alioufanya wakati akiwa Rais kabla ya Rais Jakaya Kikwete kurithi kiti chake.


Source: Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment