Pages

September 23, 2011

Kampeni Chadema, CCM zafika pabaya

Mbunge wa Tabora Mjini Ismail Aden Rage akipanda jukwaani kumnadi mgombea wa CCM Jimbo la Igunga Dalali Peter Kafumu.  

JOTO la uchaguzi mdogo katika Jimbo la Igunga, mkoani Tabora linaendelea kupanda baina ya vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo, huku kampeni zinazoendelea zikichukua sura ya mapambano baina ya vyama viwili vikubwa nchini, CCM na Chadema.Katika kile kinachoonekana kuwa hofu kadri siku ya uchaguzi inavyokaribia, jana CCM kupitia Katibu Mkuu wake, Wilson Mukama, kiliendeleza tuhuma dhidi ya Chadema ambacho kwa upande wake kilijibu mapigo kupitia kwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

 Mukama akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Igunga, alitoa tuhuma nzito kwa Chadema, akisema chama hicho kikuu cha upinzani nchini, kimeingiza kundi la makomandoo 33 kwa lengo la kuvuruga uchaguzi.

  Katibu Mkuu huyo aliyekuwa akizungumzia tathmini ya kampeni za uchaguzi huo mdogo, alitumia muda mwingi kukizungumzia Chadema, huku akivisahau vyama vingine sita ambavyo pia vinashiriki uchaguzi huo.

 Hata hivyo, Mbowe akizungumza na Mwananchi alijibu tuhuma hizo kwa kumshangaa Mukama na kueleza kuwa kauli zake katibu mkuu huyo wa CCM ni matokeo ya “kushiriki siasa za uzeeni”."Sasa hili Mukama hawezi akajua kwa sababu yeye anafanya siasa za uzeeni. ..Yeye (Mukama) hajawahi kugombea udiwani, uenyekiti wa mtaa, ubunge au nafasi yoyote ndani ya chama chake zaidi ya huu ukatibu mkuu ambao alipewa tu.. atayajuaje hayo?" Alihoji na kuendelea:

Source: Mwnanchi

No comments:

Post a Comment