Pages

September 19, 2011

Igunga kumekucha, Mabalozi CCM wanaswa wakiandikisha wapiga kura.


Nghoboko Masele aliyejitambulisha kama balozi wa nyumba kumi kumi wa CCM, katika kijiji cha Mwayunge Mashariki Kata ya Igunga, akiwa chini ya ulinzi baada kukamatwa na wafuasi wa chadema akiorodhesha majina na namba za shahada za wapiga kura pamoja na namba za simu zao katika jiji hicho.jana. Picha na Fidelis Felix



WAKATI joto la uchaguzi mdogo wa Jimbo a Igunga likiendelea kupanda, Chama cha Wananchi (CUF) kimekituhumu CCM kuwa kimeanza kukusanya na kuorodhesha kadi za wapiga kura na kwamba, kimemkamata mmoja wa mabalozi wa nyumba kumi wa CCM wakati akifanya kazi hiyo.
 
Tuhuma hizo dhidi ya CCM zilitolewa jana na mgombea wa CUF, Leopold Mahona, ambazo tayari zimeshapingwa na Mratibu wa Kampeni wa CCM, Mwigulu Nchemba.
 
Akiwa katika kijiji cha Imalilo, Kata ya Nguru, jimboni humo, Mahona alisema kazi kuorodhesha majina ya wapiga kura na kadi zao inaratibiwa na kusimamiwa na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM.
 
Mahona aliwataka wakazi wa kijiji hicho kukataa mpango huo kwa kutotoa vitambulisho vyao vya kupigia kura, kwani wakikubali kufanya hivyo watashindwa kuchagua mwakilishi mwenye uwezo wa kuwasaidia.
 
Kauli ya Mahona imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa CUF Taifa,  Profesa Ibrahimu Lipumba, kuwataka wakazi Igunga kujiandaa kukabiliana na hujuma zinazotarajiwa kufanywa na CCM kwa lengo la kulazimisha ushindi, kutokana na chama hicho kupoteza mvuto kwa wananchi.
 
"Wakija kuwaomba shahada kataeni, hata wakiwatisha msikubali, mkae kimya na msiwafanye chochote. Subirini siku ya kupiga kura na mnichague mimi nikaletee maendeleo,’’ alisema Mahona.
 
Mahona alidai kuwa, wajumbe hao wanawatisha wakazi wa jimbo hilo wanaounga mkono upinzani na kulaani kuwa, kitendo hicho kinakwamisha maendeleo na juhudi za mabadiliko ya kidemokrasia.
 
Hujuma sehemu mbalimbali
 
Wakati mgombea huyo wa CUF akilalamikia kitendo hicho, mwandishi wa habari hizi imeshuhudia tukio la uandikishaji kadi hizo ukiendelea katika maeneo mbalimbali.
 
Mwandishi alishuhudia kijana mmoja, mkazi wa kata ya Iborogero, nje kidogo ya mji wa Igunga akiorodhesha majina ya wenye vitambulisho vya mpiga kura pamoja na namba za vitambulisho vyao vya mpigakura.
 
Kijana huyo alipoulizwa na Mwananchi, huku akisita kutaja jina lake, alisema kazi hiyo amepewa na wakubwa wake ambao alikataa kuwataja na kusisitiza kuwa, anachofanya ni kuorodhesha majina ya wapiga kura na vitambulisho vyao kupigia kura kisha kuviwasilisha kwa wakubwa.
 
‘’Mimi kazi yangu kukusanya taarifa za watu wenye vitambulisho vya mpigakura. Ninaandika majina yao pamoja na namba ya kitambulisho nawasilisha kwa wakubwa, wao watatoa maelekezo na hatua za kuchukua,’’ alisema kijana huyo.
 
Mmoja watu waliotoa kadi zao, Chiristina Kaloli, mkazi wa Iborogero alipoulizwa na gazeti hili alikiri kuwa, kadi yake imeishaandikishwa mjumbe wa CCM huku kusisitiza kuwa hiki ni kipindi cha mavuno kwao.
 
Kadi hiyo ambayo mwananchi iliona kumbukumbu zake Ikiwa na namba 05262605 inaonyesha kuwa, ‘Chritina Kaloli alijiandikisha kuwa mpiga kura Desemba 26, 2004 katika Shule ya Msingi Mpogoro, Wilaya ya Igunga’.
 
CCM wakanusha
Mratibu wa kampeni wa CCM, Nchemba alipoulizwa juu ya tuhuma hizo alisema ni kitu kisichoweza kufanywa na CCM.
 
"Hivyo vyama vingine vinatapatapa, sisi ndio wenye wanachama wengi Igunga, tukifanya hivyo tutakuwa tunapunguza wapiga kura wetu, hatuwezi kufanya hivyo bali wao,’’ alisema.
 
Alisema kitambulisho ni mali ya mwenye nacho na kwa mujibu wa sheria za nchi, hakuna mtu anayeruhusiwa kuchukua kitambulisho cha mtu mwingine.
 
Nchemba alisisitiza kuwa, suala la kukusanya vitambulisho vya wapiga kura linaw....
ifuate hapa.

No comments:

Post a Comment