HALI ya siasa
katika jimbo la Igunga mkoani Tabora imechafuka baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo,
Fatuma Kimario kudaiwa kukutwa na viongozi wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akifanya
mikutano ya ndani na viongozi wa matawi, vijiji na kata kinyume cha utaratibu.
Tukio hilo la aina yake liliibuliwa kwa viongozi wa
Chadema baada ya kuonyeshwa alama ya chama chao na kijana
mmoja, Juma Gwala ambaye ni
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kitongoji cha Zahanati, kuonyesha alama
inayoonyesha matusi dhidi ya
msafara wa viongozi wa Chadema.
Hali hiyo ilisababisha walinzi wa Chadema na Mbunge wa Maswa Mashariki kwa tiketi
ya Chadema, Sylvester Kasulumbayi na Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Kiwanga
kumkimbiza.
Lakini aliwazidi mbio na kutokomea kusikojulikana.
Baada ya hapo, viongozi na walinzi wa Chadema walirudi kuendelea
na mkutano wao ambao ulikuwa umbali wa mita zipatazo 60 kutoka mkutanoni.
Wakati mkutano huo ukiendelea, ghafla kijana mmoja ambaye
hakufamika, alipaza sauti na kusema DC yuko kwenye ofisi za kijiji, huku akidai
kuwa anagawa fedha kwa viongozi wa vijiji.
Hali hiyo
ilizua mtafaruku na kusababisha watu wengi kukimbilia kwenye ofisi hizo
na kumkuta DC Kimario akiwa na viongozi
na wazee maarufu wa eneo
hilo.
Walimtia misukosuko ya hapa na pale, huku wakimpiga makofi
hadi wakamtoa nje ya ofisi.
Baada ya watu mbalimbali kuingia ndani ya ofisi, walimkuta
DC Kimario akiwa na msaidizi wake ambaye ji a lake halikutambulika, wakiwa na
nyaraka mbalimbali zinazoonyesha ajenda za kikao hicho.
Miongoni wa ajenda hizo ni uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Igunga, kuhakikisha
wageni wanaoingia kijijini au kitongojini taarifa zinatolewa kwa mtendaji wa kijiji.
TIMU ya kampeni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeingia katika msukosuko mkubwa wa chini kwa chini baada ya kiongozi mmoja mwandamizi anayeongoza kampeni hizo (jina tunalihifadhi) kudaiwa kufumaniwa na mke wa mtu, Tanzania Daima limebaini.
Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata kutoka vyanzo vya kuaminika katika Ofisi Ndogo za CCM Makao Makuu jijini Dar es Salaam na kutoka Igunga zinaeleza kuwa tukio hilo limesababisha kujeruhiwa vibaya kwa mwanamke huyo.
Ofisa mmoja wa juu wa CCM aliyezungumza na Tanzania Daima kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini alisema sakata hilo lilianza baada ya mume wa mwanamke anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kigogo huyo anayeongoza kampeni za chama hicho kuvamia chumba ambacho watuhumiwa hao walikuwamo na kuanza kumwadhibu mkewe kwa kipigo.
Kwa mujibu wa ofisa huyo, wakati vuta nikuvute kati ya mke na mume ikiendelea chumbani, kigogo huyo wa CCM alifanikiwa kutoroka na kuwaacha wanandoa hao ambao wote wawili ni makada wa CCM wakiendelea kupambana.
Habari zinaeleza kwamba mtafaruku huo ulimsababishia mwanamke huyo aliyekuwa miongoni mwa kundi la mabinti wapatao 10 wanaotumika kuhamasisha kwenye kampeni hizo majeraha makubwa yaliyomlazimisha apelekwe hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Chanzo kingine cha kuaminika cha habari kililieleza gazeti hili kwamba kabla ya kwenda hospitalini, mwanamke huyo alilazimika kupita katika kituo cha polisi cha Igunga ili akapatiwe fomu maalum ya idhini ya matibabu (PF3).
Inaelezwa kwamba mara baada ya kufikishwa kituoni hapo na wasamaria wema, mwanamke huyo (jina tunalo) alitakiwa kwanza kulitaja jina la mtu aliyemsababishia majeraha hayo na akajikuta akipata wakati mgumu kumtaja mumewe.
Habari zinaeleza kwamba taarifa za tukio hilo zilipofika katika ofisi za CCM wilaya ya Igunga, maofisa wa chama hicho waliingilia kati na kuamua kulizima jambo hilo chini kwa chini ili kuepukana na hatari ya kuvuruga kampeni nzima za ubunge cha chama hicho.
“Ni kweli tumepokea habari za kusikitisha kuhusu kiongozi wetu mmoja wa juu katika kampeni kukumbwa na kashfa ya kufumaniwa na kusababisha mwanamke aliyadaiwa kuwa na uhusiano naye kupata kipigo kikali kutoka kwa mumewe ambaye pia ni kada maarufu wa
No comments:
Post a Comment