Pages

September 22, 2011

Huruma, Upendo na Utu wetu vimeenda wapi???




Wakazi wa jiji la Dar ni nini kimetokea na kutufanya tusiwe na huruma, upendo na imani kwa wenzetu?

 Sijui ni kitu gani kimetokea ama kinaendelea jijini kiasi cha watu kukosa huruma kwa watu wengine, kujipenda ama ubinafsi umepitiliza kusema ukweli, hivi sasa anapanda mama mjamzito au ana mtoto pengine mlemavu au mzeee katika daladala hakuna hata mtu anajitingisha kumpa siti, wengine watajifanya hawajamuona, wapo watakaojiinamia kitini, saana akijitokeza msamaria mwema atampokea mama mtoto, basi. 

Lakini je ni nani awezaye kumpokea mama ujauzito wake ama ulemavu au umri wa mtu mwingine? kina mama ambao pengine ndio wangekuwa mfano wa huruma kwa wenzao kwa kuwa bila shaka wamepata kupitia hali hiyo, ndo kwanza ujifanya hawawaoni wenzao, mara nyingi kina mama hawa hupata msaada toka kwa kina baba zaidi kuliko kina mama. 

Wakati wa UDA, kwa wale ambao wana kumbukumbu nzuri au walikuwepo, kulikuwa na matangazo ndani ya mabasi, moja wapo, mbali na lile la pale mbele kwa dereva lisemalo “Basi hili limenunuliwa nusu millioni”, mengine yalikuwa yakiimiza heshima na utii katika basi, yapo yalokuwa yameandikwa “mpishe kiti mlemavu, mzee, mama mjamzito na mwenye mtoto”, nakumbuka kusoma haya nyakati zile, kwa wenzetu waliondelea ambao tunasema twanakiri toka kwao haya bado yapo, mabasi yao yana sehemu maalumu ya walemavu, mama wenye watoto, ujauzito na wazee pia. 

Hivi sasa kila kitu tunasingizia ufisadi, je hili nalo lina mkono wa mafisadi? kwamba wamechukua huruma yetu, imani na upendo wetu wa kale na kutuachia ubinafsi, choyo na kujipenda kupita kiasi? kwamba umetufanya tusahau utu wetu na ubinadamu wetu? hapana, siamini hilo. Japo kuna ukweli kiasi kuwa chanzo cha matatizo mengii yatupatayo sasa kiini chake utakuta ni ubinafsi, lakini kwa hili tuwe na huruma na ubinadamu japo kidogo.    

Kina mama hawa (pichani) walishika bomba kutoka Magomeni mpaka Mbezi, huku kina mama, baba na hata wanafunzi wamekaa vitini kana kwamba hawawaoni, hakuna anayejari, labda ifike mahali SUMATRA waagize daladala kutenga sehemu maalumu kwenye magari yao kwa makundi haya maalumu hili kupunguza usumbufu kwao.

Haya ni maoni yangu, je wewe una maoni gani?
  

No comments:

Post a Comment