Pages

September 9, 2011

CHADEMA yazindua kampeni Igunga



 Mgombe ubunge kupitia CHADEMA Joseph Kashindye akimwaga sera


KATIKA siku ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga, jana Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilitikisa mitaa na vitongoji vyote, huku mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, akitangaza rasmi kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) ni janga la kitaifa.

 Uzinduzi huo ulianza kwa maandamano yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa wafuasi wa CHADEMA walioupamba kwa vifijo na nderemo, kuanzia saa 9.20 alasiri, wakiongozwa na magari, baiskeli na pikipiki zilizopambwa na rangi za bendera ya CHADEMA.

 Viongozi wakuu wa chama hicho, akiwamo Mbowe, Dk. Willibrod Slaa, na wabunge wa CHADEMA walipokelewa na umati wa wana Igunga na kuongoza maandamano yaliyoanzia kijiji cha Hanihani hadi Uwanja wa Sokoine, ulikofanyikia mkutano mkubwa wa hadhara.

 Msafara wa CHADEMA ulisababisha baadhi ya wananchi kuacha shughuli zao kwa muda wakajiunga na maandamano hayo huku wakikishangilia chama hicho.

 Baada ya uwanjani, zilianza dua kutoka kwa viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo, kabla ya viongozi kuanza kusalimia wananchi.

 Mbunge wa Mbeya Vijijini, Joseph Mbilinyi (Sugu), alikuwa kivutio kikubwa jukwaani na kushangiliwa kwa nguvu alipokuwa akitoa salamu kwa wananchi.

 Katika hotuba yake, Slaa aliwaambia wananchi kwamba CCM imewadharau wananchi wa Igunga kwa kumtuma Rais mstaafu Benjamin Mkapa kuzindua kampeni zake, kwani naye ni gamba ambalo CCM inapaswa kuachana nalo kama ilivyofanya kwa Rostam Aziz aliyejiuzulu ubunge wa Igunga kwa shinikizo la makundi ndani ya chama chake.
 

Alisema Mkapa naye ni fisadi, kwani alipokuwa Ikulu alifanya biashara katika ofisi hiyo ya umma bila kulipia pango na alishiriki ufisadi mkubwa unaowafanya wananchi waishi maisha ya shida.

 Aliwataka wana Igunga kumchagua mgombea wa CHADEMA, Joseph Kashindye, na kumpuuza wa CCM, Dk. Peter Kafumu, kwani huyu wa CCM hawezi kuwatetea, maana anaogopa kuanika udhaifu wa serikali yake inayotafuna mabilioni ya fedha kwa manufaa ya wachache.

 Dk. Slaa alisema Rais Mkapa ni miongoni mwa vyanzo vya uhaba wa umeme uliopo hivi sasa, maisha magumu kwa wananchi na matatizo lukuki yanayowakabili Watanzania; akawataka wananchi wambane kwa maswali magumu atakapopanda jukwaani leo kumnadi mgombea wa chama hicho tawala....

Source  Tanzania Daima
Picha kwa hisani ya Mitandao

No comments:

Post a Comment