Pages

August 9, 2011

Serikali yachimbia mkwala makampuni ya mafuta..


Sehemu ya tamko la serikali lililotolewa na Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja kufuatia hoja binafsi ya Mbunge wa Bumbuli juu ya mgomo wa wauza mafuta uliodumu kwa takriban wiki sasa. 
1.                Mheshimiwa Spika, kufuatia hali iliyojitokeza, EWURA imetoa Compliance Order kwa makampuni manne ambayo ni BP, Engen, Oilcom na Camel Oil, ambapo wanatakiwa watekeleze hatua zifuatazo:
(i)            Mara moja wanatakiwa kuanza kutoa huduma katika maghala yao ikiwa ni pamoja na kuanza kuuza mafuta katika vituo vya rejareja ikiwemo vituo vilivyo chini ya miliki zao;
(ii)          Waache mara moja kitendo chochote kitakachosababisha upungufu wa makusudi wa mafuta ya petroli katika soko la Tanzania; na
(iii)        katika kipindi cha masaa 24 wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria dhidi yao kwa kukiuka matakwa ya Sheria ya Mafuta pamoja na Sheria ya EWURA.

2.                Mheshimiwa Spika, baada ya kuisha kwa muda uliotolewa na EWURA, adhabu stahiki zitatolewa kwa wahusika ikiwa ni pamoja na kusitisha ama kufuta leseni.

3.                Mheshimiwa Spika, katika hali ya kawaida na kwa mujibu wa Sheria, mtu asiporidhika na maamuzi ya EWURA anapaswa kukata rufani katika Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal). Hatua hii haijafuatwa hadi sasa na Serikali ingeshauri kwamba masuala kama haya ni vema yakafuata taratibu za kisheria.

4.                Mheshimiwa Spika; naomba kuwasilisha.



Msaada kwa wadau: COMPLIANCE ORDER yamaanisha nini kwa kimatumbi? 

No comments:

Post a Comment