Pages

August 10, 2011

Mti mkavu aagwa, JK aongoza waombolezaji

Amiri Jeshi mkuu Rais Jakaya Kikwete akitoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Luteni Jenerali Silas Mayunga "Mti Mkavu"
Mwili wa Luteni General Silas Mayunga unatarajiwa kusafirishwa kesho kuelekea Maswa mkoani Shinyanga ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika keshokutwa. 


Wasifu wa "Mti Mkavu"

Luteni Jenerali Silas Peter Mayunga alizaliwa Maswa, Shinyanga mwaka 1940. Alijiunga na Jeshi la Tanganyika Rifles Januari 10, mwaka 1963, baada ya kumaliza elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari ya Bwiru, Mwanza.
 
Alihitimu kozi ya Uofisa wa Jeshi Julai 26, 1963, nchini Israel, akahitimu kozi ya Unadhimu na Ukamanda wa Jeshi mwaka 1973 nchini Canada na kuhitimu kozi ya Ukamanda wa Juu wa Jeshi mwaka 1974 hapa nchini.

Alipandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali Juni 21, mwaka 1995 na kabla ya kustaafu jeshini Desemba 31, 1995, alipata kuwa Mkurugenzi wa Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi, Mkurugenzi wa Tawi la Mafunzo Makao Makuu ya Jeshi, Kamanda wa Brigedi ya 202 ya Tabora, na Kamanda wa Divisheni za 20 na 30 za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Jenerali Mayunga alishiriki kikamilifu Vita Dhidi ya Iddi Amin katika Operesheni Chakaza ambako alikuwa Kamanda wa Brigedi ya 206 na baada ya hapo kuwa Kamanda wa Kikosi Maalum cha JWTZ nchini Uganda kati ya 1979 na 1980.

Mbali na jeshi, Jenerali Mayunga alitumikia umma kama Mkuu wa Mkoa wa Singida mwaka 1977 – 1978, Katibu wa Chama wa Mkoa wa Kilimanjaro 1983-1988, Balozi wa Tanzania katika Nigeria kati ya 1989 hadi 1998 na Balozi wa Tanzania katika DRC kati ya 1998 na 2002 alipostaafu utumishi wa umma.         

RIP Mpiganaji na shujaa Jenerali Mayunga

No comments:

Post a Comment