Pages

August 12, 2011

Kumbe ni rahisi kuondoa traffic jam jijini.


 Siku zile wauza mafuta walipogoma kuuza mafuta, magari na hasa binafsi yalihadimika barabarani, safari ya Mbezi mpaka katikati ya jiji ilikuwa yachukua dakika kadhaa na si masaa kadhaa kwa kutumia  usafiri wa umma ambao haukuwa na kasheshe sana kama ilivyozoeleka.

Hivi leo baada ya hali ya upatikanaji mafuta kurejea katika hali yake ya kawaida, barabara zimefungamana tena, asilimia kubwa ni magari binafsi ambayo waweza kuta kuna mtu mmoja saana wawili na usafiri wa umma umekuwa ni kasheshe tena, kwanini????????



Nimejifunza jambo hapa, (though the hard way) kumbe tukiweza kudhibiti magari binafsi na kuboresha usafiri wa umma na kuwasimamia barabara watoa huduma tunaweza kuondoa foleni hizi zisizo za lazima jijini ambazo zinasemekana zinasababishia taifa hasara ya Tsh Billioni 4 kila siku! Taifa changa na masikini kama hili kupozea mahela yoote hayo kwa sababu ya kushindwa kufanya japo maamuzi madogo kama haya haiingii akilini.

 Labda tatizo kubwa hapa ni ubinafsi, maana wenye magari ni sisi wenyewe ambao ndio tunapaswa kuamua, sababu kuu ni kuwa twajifikilia sisi kwanza.  

No comments:

Post a Comment