Pages

August 23, 2011

Jairo arejeshwa kazini!


"Uchunguzi uliofanywa na CAG umeonesha kuwa tuhuma zilizotolewa bungeni Julai 18 hazikuweza kuthibitishwa, kutokana na matokeo hayo ya uchunguzi wa awali mimi kama mamlaka ya nidhamu ya Katibu mkuu Nishati na Madini Bw David Jairo, sitaweza kuendelea na hatua ya pili ya kumpa taarifa ya tuhuma (notice) na hati ya mashitaka kwa sababu hajapatikana na kosa la kinidhamu kwa mujibu wa taarifa maalum.
 
Kufuatia matokeo hayo ya taarifa hii ya awali na kwa mamlaka niliyonayo kwa mujibu wa sheria namba 8 ya utumishi wa umma ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003, Ninaamuru Bwana David Kitundu Jairo arejee kazini kuanzia siku ya Jumatano tarehe 24 Agosti 2011."  

Philemon Luhanjo,
Katibu Mkuu Kiongozi

No comments:

Post a Comment