Pages

July 18, 2011

Breaking nyuuuuuuuuuuz!! Ngeleja akwaaa kisiki

Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini imekwama kupita na kusogezwa mbele kwa muda wa wiki tatu ili  kutoa majibu muafaka kuhusu mgao wa umeme pamoja na mambo mangine.

Hoja ya kuhairisha bajeti hiyo imetolewa na Kiongozi wa Serikali Bungeni Waziri mkuu Mizengo Pinda, bunge bila kujari itikadi za vyama limepitisha kwa kauli moja hoja hiyo.

Pengine hii yaweza kuwa dalili njema kwa siasa za Tanzania kwa Wabunge kuungana kwa pamoja na kuwa na sauti moja katika mambo au matatizo yanayohusu taifa na kugusa wananchi moja kwa moja.


Huu ni ukomavu wa kisiasa unaotakiwa kuoneshwa katika mijadala yote.

No comments:

Post a Comment