Pages

June 25, 2011

Dharau hizi zakujitakia, tumezinunua kwa gharama sana




Hii aibu, dharau na kutoaminiwa ni  vya kujitakia, wala tusiwalaumu hao wanaodhani kuwa hatuna uwezo wa kutumia vyema fedha zetu vizuri.  


Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe alinukuliwa jana bungeni akisema "Tanzania ni nchi maskini, lakini haiko tayari kudharauliwa kiasi hicho kwa serikali yake, tasisi zake na asasi zake kutoaminiwa. kuruhusu hilo lifanyike ni kuruhusu kuibiwa kwa mara ya pili,"alisema Membe.


Hivi sasa ujumbe mkubwa wa watu nane ukiongozwa na Naibu Spika Jobu Ndugai huko Uingereza kujaribu kuwaomba BAE wasipitishie kwa mashirika yasiyo ya kiserikali chenji yetu tulolanguliwa ama tulojitakia kulanguliwa na kwamba ipitie serikalini ambapo “wanasema” itaenda kuboresha elimu (je pasingekuwepo chenji hii elimu isingeboreshwa? Sina hakika)



Yes, hakuna mwanadamu huru duniani kote anayependa kudharauriwa, sembuse serikali ama Taifa! Lakini yapo matendo ambayo kwa hakika uwezi kumlaumu yule anayekudharau bali yabidi yabidi kujirudi na kujitazama kwanini ufikiwe kudharauriwa na awaye yote yule, utagundua kumbe ni matendo yako yamepelekea dharau ama kutoaminiwa huko, nadhani ndivyo ilivyo kwa sakata hili la rada na na Kampuni ya BAE System ya UK.

Je kama Taifa au Serikali hatukujua? Au hatukuonywa juu ya dili hili? Ikiwa tulionywa ama kujuzwa juu ya dili bomu hili, Je nini kilitu(wa)sukuma tukalazimisha ununuzi huu kwa bei ya KURUSHWA na RUSHWA?

Benki ya Dunia pamoja na IMF walikataa kutoa pesa kwa DILI hili, kisa walisema ni bei ya kulangua, Waziri wa Mambo ya Nje wa UK wakati huo Clare Short alipinga kwa nguvu zote DILI hili, mkopo ulitoka Barclays, kwanini? Bado hili lachunguzwa pia huko UK.

“The World Bank and the IMF had refused to fund the deal, which they regarded as a white elephant. The bank said a civilian radar system could be bought at a fraction of the price. Barclays's role was heavily criticised by Clare Short, while Norman Lamb MP suggested it may have arranged the loan in return for the granting in October 2000 of a banking licence to operate in Tanzania.”

Clare Short anasemaje “My problem was that the increased aid would end up paying the BAE bill.”  Je hivi sivyo ilivyokuja kuwa baadaye?
Nukuu ingine toka kwa Clare Short, “The local representative of the World Bank therefore asked the International Civil Aviation Organisation to report on the project. The report said that the system was very old technology and was military, not civil. Tanzania had no use for such a system. It did need better civil air traffic control to improve tourism. A loan was available from the European Investment Bank to install a state-of-the-art system for Tanzania and its two neighbours that cost less than half the BAE system.”
Baada ya Benki ya Dunia na IMF kukataa na kutilia shaka dili hilo waziri wetu wa Mambo ya Nje wakati huo alinukuliwa akisema  "We are not a department of the World Bank - we are a country and it's a bit insulting to suggest that we need to wait for the World Bank to prescribe what's best for us."

Ni wazi tuliamua kutia pamba masikioni, hatukutaka kusikia wala kuambiwa, wapo waliopigia sana debe rada hii kuwa ni lazima inunuliwe hata kama itabidi tule nyasi, japo kuna waliopinga na ata kuleta bei mbadala ambayo ni nusu ya ile iliyotakiwa kulipwa kwa mujibu wa mitandao lakini walipuuzwa, leo hii tunaposema kuwa hutukotayari kudharauliwa au kupuuzwa je twamaanisha kweli? Je tumeshasahau miaka kumi tu hii nini tulifanya? Je leo hii hatuwajui waliotufikisha hapa?  Tumeshawasahau, hatuwakumbuki ama hawajulikani? WENZETU wanawajua,      Haya mengine kwakweli twajitakia, tukubalia au tukatae.

No comments:

Post a Comment