WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesikitishwa na maisha wanayoishi wanafunzi wa Shule ya Msingi Mulusagamba iloyopo wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera.
Pinda alionyesha masikitiko hayo jana baada ya kufika shuleni hapo na kuwaona wanafunzi wa shule hiyo wakitembea bila viatu huku sare zao za shule zikiwa chafu.
Waziri Mkuu huyo ambaye yuko katika ziara ya kiserikali katika Mkoa wa Kagera, alifika katika shule hiyo kwa ajili ya kupokea taarifa ya maendeleo ya Wilaya ya Ngara iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Salumu Nyakonji.
”Hali walionayo wanafunzi hawa ni mbaya sana kwani inaonekana kuchangiwa na umaskini unaowakabili wazazi wao.
“Ili kuondokana na hali hii lazima sasa viongozi wa wilaya muwe wabunifu, mbuni fursa mbalimbali zitakazowaongezea wananchi wastani wa kipato chao.
“Viongozi lazima mhakikishe wananchi wanaboresha kilimo ili kiwe na tija kwani kwa kufanya hivyo wataweza kukabiliana na umaskini wa kipato unaowakabili,” Alisema Pinda
Ili kuimarisha Kilimo Kwanza, aliwataka viongozi wilayani hapa wawahamasishe wananachi juu na manufaa ya kilimo cha kisasa kwa kufuata kanuni za kilimo.
Pages
▼
No comments:
Post a Comment