Pages

February 17, 2011

"Goms" si salama tena!

Wakati Makamu wa Rais Dr Ghalibu Bilali akioneshwa sehemu mabaki ya mabomu yaliyolipuka jana usiku, wakazi wa maeneo hayo wako kwenye pilika pilika za kuondoka maeneo hayo wakitafuta hifadhi popote watakapo pata, wengi wanaamini kuwa mabomu hayo uenda yakalipuka tena kama ilivyokuwa Mbagala hivyo ni heri nusu shari kuliko shari kamili.
Taarifa zimekuwa zikitolewa kuwa kuna watoto wengi wamepotea, wengi wako vituo vya polisi, uwanja wa Uhuru na Sabasaba, wito umetolewa waliopotelewa kwenda kuangalia ndugu na jamaa zao sehemu hizo.
Mpaka sasa idadi rasmi ya waliopoteza maisha kutokana na milipuko hiyo ya jana haijatolewa, inakisiwa kuwa wanaweza kufika mia moja, Waziri Mkuu amenukuliwa akisema ni zaidi ya ishirini na Mnadhimu Mkuu wa jeshi alinukuliwa na bbc kuwa ni 32, hakuna idadi rasmi mpaka sasa.
Tunawapa pole wale woote waliofikwa na majanga haya, waliojeruhiwa, waliofiwa na ndugu na jamaa zao pia, na zaidi tunawaombea heri marehemu wote, Mungu alaze roho za marehemu hao pema peponi. Amen.
Picha kwa hisani ya John Bukuku.

No comments:

Post a Comment