Pages

January 21, 2011

Kisa cha Ngombe, Mzee na mtoto mwenye hekima

Niliwai kusoma hadithi hii mahali fulani, kwa bahati isiyo njema sikumbuki ni kitabu gani, anyway hadithi yenyewe iko hivi:-
Mzee mmoja mfugaji akiwa na mwanae mdogo alikwenda kuchunga mifugo yake wakiwamo Ng'ombe kadhaa, katika kundi lile ng'ombe mmoja alizaa kandama hukohuko polini, ilipofika jioni ilibidi kuwarudisha mifugo yake zizini, wote waliongoza njia isipokuwa yule ngombe na ndama wake, ndama yule baada ya miguu yake kupata nguvu alikuwa anarukaruka tu kule polini.
Mzee yule alikuwa akiangaika kumchapa ngombe mzazi ili aongoze njia ya zizini lakini ngombe yule hakuwa tayari kwani ndama alikuwa bado akivinjali polini kule, Mzee aliangaika kwa kitambo bila mafanikio huku mwanae akimwangalia tu.
Mwishoe mtoto akamshauri babaye, akamwambia- "Baba kwanini usimbebe yule ndama? kwani mamaye atakufuta tu"
Mzee akumwelewa kwanza mtoto wake aliendelea kidogo kumlazimisha ngombe wake, mwishoni akaamua kujaribu kufuata ushauri ule lakini kwa namna ya kujifanya yeye ndo kaamua, akambeba ndama na hatimaye ng'ombe naye akamfata mpaka zizini.
Jambo lile la kushauriwa na mtoto wake tena wa miaka kumi tu lilimkwaza sana mzee yule alifikiri saaana mwishowe akafanya kitendo cha kijinga, akaamua kujinyonga, kisa, kushauriwa na mtoto mdogo.
Sitarajii baba zetu nao watafanya kitendo cha kijinga kama cha mzee mfugaji yule, sitarajii, nina hakika baba zetu leo hii wanabusara sana, wataona ushauri wa mtoto ni changamoto ya kujitafakari na kuamua kwa busara zaidi sasa na wakati ujao pi.
Hongereni sana VIJANA kwa kukataa kukaa kimya.

2 comments:

  1. Anonymous4:46 PM GMT+3

    Asante kwa hadithi ambayo sijaielewa wasomaji wake ni wa chuo kikuu . shule ya sekondari. msingi au hadithi za watoto wachanga. Samahani sana .na nakushauri urudi darasani kaendelee kusoma ongeza elimu utapata faida. halafu urudie kusoma hadithi hiyo naamini utaiandika upya kutokana na elimu uliyomaliza.

    ReplyDelete
  2. Anonymous4:49 PM GMT+3

    Asante kwa hadithi ambayo sijaielewa wasomaji wake ni wa chuo kikuu . shule ya sekondari. msingi au hadithi za watoto wachanga. Samahani sana .na nakushauri urudi darasani kaendelee kusoma ongeza elimu utapata faida. halafu urudie kusoma hadithi hiyo naamini utaiandika upya kutokana na elimu uliyomaliza.

    ReplyDelete