Pages

December 1, 2010

UMASIKINI au UTAJIRI ni maamuzi binafsi?

Ukiangalia mchoro huu wa Msanii Maembe kwa haraka uwezi kuona picha iliyopo hapo, lakini ukitulia ukaangalia tena na tena utaona picha fulani hapo ambayo waweza itafsiri upendavyo na mara utakapoziona picha hazitaondoka akilini, kila uangaliapo mchoro huo zitakujia haraka sana.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa fursa nyingi na hasa katika ulimwengu huu wa ICT tuishimo, si rahisi mtu kuona fursa mahali fulani hata kama utamlazimisha vipi, ni mpaka pale atakapoamua mwenyewe kuangalia tena na tena ndipo ataiona.
Biblia yasema- "Mauti na Uzima huwa ndani ya uweza wa ulimi,"
Je si ni sahihi pia kusema UMASIKINI na UTAJIRI huu ndani ya uweza wa ULIMI?
Je si ni kweli kufa masikini ni uamuzi wa mtu?
Waweza jitamkia UZIMA na UTAJIRI ungana na walio AMUA kuukataa umasikini HAPA

No comments:

Post a Comment