Pages

November 27, 2010

Je wewe uko kundi gani? Which group do you belong?

Je uko kundi gani?

Dunia ya utafutaji/kipato binadamu tumegawanyika katika makundi makuu manne, kwa mujibu wa Msomi, Mfanyabiashara, Mwamasishaji na mwandishi wa vitabu wa Marekani Robert Kiyosaki, nayo ni 1. Mwajiriwa, 2. Kujiajiri, 3. Mmiliki wa Biashara na 4. Mwekezaji.

Robert Kiyosakim katika kitabu chake cha Rich Dad’s Cashflow Quadrant ameyagawa makundi haya mane katika pande kuu mbili, Kushoto kuna 1 & 2 na kulia ambako kuna 3 & 4.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali duniani Upande wa kushoto wa Waajriwa na Wanaojiajiri, ndio wenye idadi kubwa ya watu 80% lakini unamiliki asilimia 5% ya utajiri wa dunia, na upande wa kulia, Wamiliki Biashara na Wawekezaji una aslimia 20% tu ya idadi ya watu wote lakini unamiliki asilimia 95% ya utajiri wa dunia.

Vitabu vitakatifu vinakili kuwa Mungu hakutuumba tuwe masikini, ndio maana kabla ya kuumbwa kwa mwanadamu aliandaa mazingira yote na akatupa mamlaka ya kuvitawala viumbe vyooote ikiwemo mali zote alizotuandalia iwe juu ama chini ardhini, baharini au nchi kavu. NK. Walio upande wa kulia wamejua hilo ndo maana wakafanya maamuzi sahihi.

Sifa kuu za pande zote mbili,

1. Kushoto – Waajiriwa na Wanaojiajiri

Ndilo kundi lenye watu wengi zaidi na lililo masikini pia, Ili kufanikiwa katika kundi ni lazima ama usome sana, ujinyime sana, ufanye kazi kwa muda mrefu sana nk.

Kadiri unavyofanikiwa katika kundi hili ndivyo unavyozidi kukosa muda wa kupumzika, kuwa karibu na familia yako nk.

2. Kulia – Wamiliki wa Biashara na Wawekezaji.

Hili lina idadi ya watu wachache sana duniani lakini likiwa linamiliki asilimia 95% ya utajiri wa dunia.

Kadiri unavyofanikiwa katika kundi hili ndivyo unavyopata muda mwingi wa kupumzika, unafanya kazi muda uutakao na pia unapata fursa ya kuwa karibu na familia yako kwa muda mrefu, NK

Je kwanini kundi hili la kulia linakuwa hivyo?

Jibu ni kuwa linatumia fomula ya OPT & OPM, Wamiliki wa Biashara na Wawekezaji wanatumia Other People Time na Other People Money, hivyo mafanikio yao hayategemei ufanyaji wao wa kazi, wanatumia watu wa upande wa kushoto.

Je wewe uko upande gani? Je ungependa kuwa upande wa kulia ili uweze kutumia OPT & OPM?

Ni rahisi sasa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya dunia kuama kutoka kushoto kwenda kulia, tena kwa gharama ndo sana, haijawai kutokea kukawa na DEMOKRASIA YA UTAJIRI (Democratization of Wealth) kama alivyoiita Prof wa Uchumi wa Marekani Paul Zane Pilzer.

Prof Pilzer anasema, “A great opportunity lies ahead, not just for the chosen few, but for literally millions of ordinary people, individual entrepreneurs who were not born into wealthy families, but who choose to apply themselves in the new emerging industries where this new wealth is being created”.

Ikiwa kweli wataka (wachagua) kujiondoa katika kundi la kushoto (umasikini) na kujiunga na kundi la kulia (Matajiri), na waamini kuwa inawezekana fuata kiambatanishi hapo chini.

La kama umeridhika na kundi ulilopo na wadhani haiwezekani kuondoka na umasikini, kwamba wewe ni wa hivyohivyo, ndo ulivyoandikiwa basi waweza ishia hapa.

Bofya hapa uone namna gani hii inawezekana.

No comments:

Post a Comment