Kwa kuweza kuchangisha Billion saba kwa usiku mmoja sio siri CCM (ama Katibu MkMakamba) wanastahili pongezi za dhati kabisa, sina kumbukumbu sahihi ni harambee hipi iliwahi kuchangisha pesa zote hizi kwa usiku mmoja tena ikiongozwa na Katibu wa chama tu, lakini kwa kumbukumbu ndogo niliyonayo naamini hii imevunja rekodi (niko tayari kusahihishwa) ya harambee zote.Nilikuwa najiuliza iwapo Makamba kaweza kuchangisha pesa zote hizo kwa ajili ya kampeni za chama kimoja tu? je ingekuwaje kama Waziri Mkuu angekuwa achangisha kwa ajili labda ya madawati kwa shule nchi nzima? na ingepatikana kiasi gani kama mchangishaji angekuwa ni Makamu wa rais labda kwa ajili ya vitanda na madawa hospitalini?Na je ingepatikana mabilioni mangapi kama mchangishaji angekuwa ni mwenye nchi mwenyewe yaani Rais kwa labda miuondombinu ama maendeleo ya taifa kwa ujumla?Nathani Makamba kaonesha njia kuwa kama tukiamua tunaweza kutatua matatizo yetu wenyewe kwani sisi si masikini na wala MUNGU hakuumba WaTanzania masikini ndio maana kabla hajatuumba alitundalia kila aina ya mali ardhini na baharini ili zitunufaishe sisi.Kumbe tukiamua nasema TUKIAMUA wanafunzi hawa wa Shule ya Msingi Mahanga huko Kigoma vijijini wanaweza kusoma kwa raha, lakini ni kama kweli tuna utashi wa kuamua ama tunaguswa kweli na hali hii.
Pages
▼
No comments:
Post a Comment