Pages

July 25, 2010

Natamani OLD DAR ama NEW Dar

Yawezekana nikaonekana mshamba, ama wengine kuniita wakuja au hata kudiriki kusema nimepitwa na wakati na labda kunibandika majina ya kila aina, wacha waseme ama wanikandie potelea mbali, lakini ukweli ni kwamba mwenzenu natamani sana pawe na Old Dar ama labda NEW DAR.
Ndio Dar ya zamani au labda New Dar natamani sana iwepo moja wapo, sio kwamba niko ndotoni, hapana, sioti wala sijalala, bali ndo natamani iwe hivyo.
Baadhi ama pengine wengi wetu Dar hii iliyopo imetuchosa, aina raha tena kukaa, ila twakaa tufanyeje, ndo twatafutia mkate wa kila siku, lakini waaama ipo siku kama Dar itaendelea kuwa hivi ilivyosasa nitaiama bila taarifa na mipango iko mbioni, kama hauamini shauri yako.
Kuna kero nyingi sana jijini kuliko mikoa mingine yoyote hapa Bongo, kuanzia barabarani, uwe na gari kero usiwe naro taabu, ukija kwa usafiri wa umma ni kasheshe, hakuna nafuu ya kukodi TAXI wala kupanda Daladala, sio siri wakazi wengi wa jijini hupoteza masaa mengi kwenye foleni ama kuziwazia tu kuliko kufanya kazi, ukija kwa DAWASCO na TANESCO ni balaa tupu,
wengi wetu hatuwezi kuondoka kwani ndo mitego yetu iliko tegwa.
kibaya zaidi watu wanazidi kuja kila uchao tena kwa wingi, hakuna uwiano wa ukuaji wa jiji na hupatikanaji wa huduma muhimu ama uboreshaji wa miundombinu, hii inasikitisha sana, zaidi ya yote wataalamu wetu jiji ama mipango miji hawana njia mbadala ya kukabiliana na changamoto zooote, badala yake leo hii bado wanaruhusu ujenzi holela wa migorofa katikati ya jiji pasipo kufahamu kuwa wanaongeza msongamano wa watu na magari site senta.
Unapovunja nyumba ya kawaida iliyokuwa ikitumiwa na familia moja ama mbili na kujenga jengo la ghorofa 10 mpaka 20 maana yake ni nini kwa ongezeko la watu jijini?
Sio siri mwenenu natamani sana New Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment