WAKATI wanasayansi waliogundua dawa ya Ukimwi wakiweka bayana jinsi inavyofanya kazi mwili kupambana na ugonjwa huo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa amemshukuru Mungu kwa taarifa za ugunduzi wa dawa hiyo.Taarifa ya kupatikana kwa dawa hiyo zilitangazwa mwishoni mwa wiki na wanasayansi wa Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaida) ya Marekani, akisema kuwa tiba hiyo inaweza kutibu ugonjwa huo hatari kwa asilimia 90, kiwango kinachoiweka dawa hiyo kwenye uwezekano mkubwa wa kupitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na hivyo kuanza kutumika rasmi.
Dawa hiyo huchochea mwili na kuuongoza katika kujitengenezea aina ya chembechembe za kinga zenye uwezo wa kukabili virusi vya ukimwi. Chembechembe hizo zimepewa jina la kitaalamu la VRCO1 na VRCO2 ambazo utafiti wake umeonyesha kuwa zinaweza kuvikabili virusi vya Ukimwi kwa asilimia 90.
source:Mwananchi
watanzania wenza tupigeni magoti nakumshuru mungu kwa hii habari njema kwani ugonjwa huu hakuna ambaye hajaguswa na gojwa hili itakuwa kila mtu ameguswa kwa njia moja au nyingine kwa hiyo tumshukuru mungu kwa huu mwangaza unaotaka kuonekana mungu azidi kufungua milango dawa kamili ipatikane na iweze kutibu watu mungu ni mwingi wa huruma anasikia sala ya waja wake mungu apewe sifa amina
ReplyDelete