Pages

June 11, 2010

Vuvuzela kuanza rasmi kuzizima leo.

Leo ndio leo, ilikuwa miaka, miezi, wiki, siku na hatimaye ni masaa tu kuanza rasmi kwa fainali za Kombe la Dunia huko Bondeni ikiwa ni mara ya kwanza toka kuumbwa ulimwengu kwa fainali hizi kufanyika Afrika.
Dimba hili la Soccer City ndipo ufunguzi utakapofanyikia na pia ndipo mechi ya mwisho itafanyikia.
Japo nchi yaongoza kwa uhalifu na bahati mbaya tayari kuna taarifa ya waandishi kuvamiwa na kuporwa kwa mtutu wa bunduki, (nami pia yaliwai kunikuta ktk SAA) lakini tnatumaini kuwa patakuwa na udhibiti mzuri wa usalama hili pasiwepo vitendo hivi tena.
\
Kila la kheri WOZA.

No comments:

Post a Comment