Pages

April 21, 2010

Pamoja na nyongeza 100% Mgomo uko palepale - TUCTA

SERIKALI imepandisha kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi kwa asilimia 100, huku wafanyakazi wa Serikali na sekta ya umma, wakitakiwa kuvuta subira hadi Jumapili ijayo wadau watakapokaa kujadili.
Hata hivyo, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), limesema tamko hilo la Serikali ni siasa na msimamo wao hautarudisha nyuma nia ya wafanyakazi kugoma Mei tano mwaka huu, endapo madai yao makuu matatu hayatatekelezwa kabla ya Mei Mosi.
Katika madai hayo makubwa, Tucta wanaitaka Serikali iongeze kima cha chini cha mshahara, ipunguze kodi inayokatwa katika mishahara (PAYE) na kuongeza malipo yanayotolewa na mifuko ya pensheni.
Hata hivyo, msimamo huo wa Serikali na wa Tucta umetolewa wakati taarifa za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), zikionesha kuwa kiwango cha chini cha mshahara wa Tanzania ni kikubwa kuliko Kenya na Uganda.
SOURCE: Habarileo

No comments:

Post a Comment