Pages

July 9, 2009

Miili ya WACOMORO YAWASILI DAR

Miili ipatayo 14 iliyoopolewa ktk Kisiwa cha Mafia imewasili leo hii na kupokelewa na Makamu wa Rais wa Visiwa vya Comoro Idi Nadhoin na ujumbe wake wakiwa na mwenyeji wao Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe,
Ajali ya ndege ya Yemenia Air Bus 310 ilitokea alfajili ya Juni 30 wakti ikielekea kutua ktk huko Comoro na ni msichana mmoja tu ndo aliokoka katika ajali ambapo kulikuwa na abiria wapatao 153, hii ndio miili ya kwanza kuonekana toka kutokea kwa ajali hii siku zipatazo kumi zilizopita.
Mungu awalaze mahali pema peponi marehemu wote. Ameni.

1 comment:

  1. Kweli Bahari haihifadhi chochote kisichohitajika ndani yake, niliwahi kuambiwa kuwa chochote kilichopo ndani ya Bahari ni halali kuliwa kwa kuwa kila kisichostahili ndani yake siku moja utakikuta ufukweni.

    Hapa ni miili ya ndugu zetu waliofariki kwa ajali ya ndege Mungu awasitiri madhambi yao na awape makazi yanayolingana na waliyoyatanguliza mbele yao kabla ya kukumbwa na umauti

    ReplyDelete