Pages

June 15, 2009

WAPO FM KUMBURUZA MKULO KORTINI?

Kuna habari kuwa Waziri wa Fedha na Mambo ya Uchumi, Mhe. Mustafa Mkulo yuko mbioni kuburuzwa kortini kutokana na madai ya kumwaga mitusi 'live' kwenye kipindi kimoja cha redio ya Kikristo cha WAPO FM cha Jijini Dar.

Taarifa hizo zinadai kuwa hatua ya kuanza kwa mchakato wa kumburuza kortini Waziri Mkulo, inatokana na madai hayo kuwa alimwaga mitusi kwa mtangazaji wa redio hiyo ya WAPO FM aitwaye Anthony Joseph.

Zinadai zaidi taarifa hizo kuwa hadi sasa, tayari mhusika ameshakutana na wanasheria wake kwa ajili ya kuandaa mashtaka dhidi ya Waizri Mkulo.

Aidha, inalezwa zaidi kuwa uongozi wa redio hiyo nao umeshaanza kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kumuandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saidi Mwema na kumueleza juu ya tukio hilo linalodaiwa kutokea Jumatano iliyopita.

Inadaiwa kuwa Mkulo alimwambia mwandishi huyo kuwa Watanzania wenye akili wanafuatilia bajeti kwani ndio mambo yanayowafaa na kwamba mambo ya DECI ayaulizie baada ya bajeti.

Inadaiwa kuwa mtangazaji alipojaribu kumuuliza iwapo ripoti hiyo ingewasilishwa baada ya kikao cha bajeti, Waziri Mkulo alimkatisha na kumjibu kwa sauti ya ukali kuwa ni 'stupid' (mpumbavu) na kuongeza kuwa : "... kama hilo ni muhimu kwako, jiulize mwenyewe, shenzi"

source: Alasiri

No comments:

Post a Comment