Pages

May 31, 2009

Mbunge Aloyce Kimaro apata ajali

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Aloyce Kimaro amenusurika kufa baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kuparamia mawe yaliyopangwa barabarani na kupata ajali usiku wa kuamkia jana.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Kimaro na polisi zinasema kuwa, ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mikongeni kata ya Lembeni wilayani Mwanga, Kilimanjaro kwenye barabara kuu ya Moshi-Tanga, akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda jimboni kwake.

Kwa mujibu wa habari hizo, wakati ajali hiyo inatokea, Kimaro alikuwa na rafiki yake Joseph Temu ambaye ndiye aliyekuwa anaendesha gari hilo aina ya Mercedes Benz akiwa na mkewe na watoto wake watatu. Katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa.

No comments:

Post a Comment