Pages

April 16, 2009

Mbegu zi Salama kweli????

WATEJA "wapanda Mbegu" ama "washiriki" kama wanavyotambuliwa na uongozi wa DECI wa mchezo wa Upatu maarufu kama panda uvune mbegu wamepagawa baada ya taasisi hiyo kufunga ofisi zake nchini nzima.
Wakati washiriki hao wakiwa njia panda juu ya hatima ya MBEGU ZAO kama zi salama au zimeenda na MAFURIKO, uongozi wa taasisi hiyo umeibuka jioni hii na kueleza kuwa umesitisha kwa muda shughuli zote kama njia ya kuheshimu tamko la waziri mkuu.
“Ttunafanya mawasiliano ya karibu na serikali kuondoa utata kuwa DECI Tanzania Ltd sio upatu kama tulivyotafasiriwa vibaya na kuhumiwa vibaya pasipo kusikilizwa kwanza.
“Tunapenda kuwafahamisha washiriki wetu kwamba, pesa zao ziko salama, viongozi wote wako salama, tunawaomba mtunze vizuri lisiti mpaka hapo huduma zitakaporejeshwa,” alisema Timotheo oleloiting'ye Mkurugenzi Mtendaji wa DECI.
Je MBEGU ZOTE ZI SALAMA???????

Pengine hili ndo swali kubwa kwa sasa, Kulingana na takwimu alizotoa MD huyo jana alipokuwa akiongea na ripotaz ni kuwa
  • Mbegu zilizokusanywa au KUPANDWA toka kuanza ni Bilioni 54.
  • Mbegu zilivunwa ni Bilioni 38.
  • Mbegu zilizong'olewa baada ya kuanza sintofahamu Bilioni 5
  • Mbegu SHAMBANI ni BILIONI 11

Hii ndo takwimu aliyotoa Bw Oleleiting'ye jana na kwamba hadi juzi walikuwa na "WASHIRIKI" wanaofikia LAKI SABA nchi nzima.

Je MBEGU SHAMBANI YATOSHA KUWAREJESHEA WAPANDAJI HAWA WAPATAO LAKI MBEGU ZAO?????

1 comment: