ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Biharamuro Magharibi, kwa tiketi ya Chama cha Tanzania Labour (TLP), Phares Kabuye amekufa katika ajali ya basi iliyotokea leo hii mkoani Morogoro.
Kabuye alikuwa akisafiri kwa basi la Kampuni ya RS Investment lenye namba za usajili T 934 ADA aina ya Scania akitoka mkoani Kagera kwenda Dar es Salaam kuhudhuria mkutano mkuu wa TLP kesho.
Ingawa Kamanda wa Polisi , Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye hakuthibitisha kifo cha mbunge huyo wa zamani aliyevuliwa ubunge na Mahakama Kuu, lakini Mwenyekiti wa TLP Taifa, Augustino Mrema alilithibitishia gazeti hili kuwa amekufa. Mkuu wa Wilaya ya Kilosa , Halima Dendegu, alitembelea majeruhi.
“Kabuye hatunaye tena. Nimepata pigo. Nimeongea kwa simu na motto wake aliyeko Mwanza. Sasa hivi tunatafuta simu ya motto wake aliyeko hapa Dar es Salaam tujue cha kufanya,” alisema Mrema.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema. Peponi. Amen
ReplyDeletedua,BISMILAHI RAHMANI RAHIM,RABANATILFILDUNIA,HASANATAN,WAFILAAHERA,HASANATAN,WAKINAA DAHAB,NAAL,WAKINAADHAB LAKABULA.WALHAMDULILAHIRABILAARAMINA.
ReplyDeleteAmefariki ni lugha ya ustaarabu zaidi kuliko amekufa. Amekufa hasa hasa ni kwa wanyama.
ReplyDeleteMungu amlaze marehemu mahali pema peponi