Pages

March 6, 2009

SIZITAKI MBICHI HIZI!!!!

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, Dkt. Idris Rashidi, ametangaza uamuzi wa kujitoa kwa shirika hilo katika nia ya kununua mitambo ya kufua umeme ya Dowans.
Kwa mujibu wa Rashidi, uamuzi huo umefikiwa baada ya kutolewa taarifa alizodai kuwa ni za uongo na zilizojaa utashi wa kisiasa zaidi, dhidi ya utaalamu wa Tanesco na kwamba zimechangia kuvunja nguvu ya mamia ya wafanyakazi wa shirika hilo nchini, ambao wanafanya kazi usiku na mchana, kuhakikisha nchi inapata umeme wa uhakika.
“Ni imani yetu kwamba tumeishajieleza na kujenga hoja za kutosha, na umma wa Watanzania utafanya uamuzi wao wakati nchi itakapokuwa imegubikwa na giza, hospitali hazitoi huduma, viwanda havizalishi na wanafunzi vyuoni wakishindwa kusoma,” alisema Rashid.

No comments:

Post a Comment