Bongo ndo pahala pekee duniani humu waweza fanya mambo yako kienyeji, kuanzisha mradi wowote na hata kujipendelea kwa kupoka huduma ya jamii nzima na kujimilikisha na kisha ukapanga ni kiasi gani uwalipe wahusika na asikuoji wala kukusumbua awaye yote yule na bado mambo yakakuendea bomba tu, ka ka-shamba haka ka-matanki ya maji huko Mbezi Africana na Mwekezaji huyu ambaye amejitahidi kuwekeza hapa baada ya kujinyima kweli au kulala njaa kwa jina la save bajeti.
Anasema anaweza kujipatia tulita laki na nusu tu kwa siku na kugawa kwa tujibiashara twake uto tudogo tu na kila mwisho wa mwezi ulazimika kujikamua kwelikweli kuwalipa DAWASCO libili la kumkomoa la TSHS 122,000/- , analalamika kuwa anaonewa sana na hawa jamaa kwani HILO LIBILI NI KUBWA SANA kulinga na tujimaji atumiatwo, yaani tulita laki moja na nusu tu kwa siku, zaidi soma hapa.
Hayo ndo ya huku kwetu BONGO, Ndo maana naipenda sana Bongo!!!!
Inachekesha! No comment. Maelezo yako yanajitosheleza
ReplyDelete