Pages

February 6, 2009

SHERIA DAY LEO

JAJI MKUU AMPONGEZA JK KWA KUTOINGILIA UAMUZI WA MAHAKAMA.
HAPA MIHIMILI MITATU NA WANNE USIO RASMI (yaani mie) IMEKAMILIKA.
Sherehe za siku ya sheria kuashiria kuanza kwa mwaka wa kimahakama zimefanyika asubuhi hii na kuudhuriwa na Mh Rais JK na Spika Sitta.

“Awali ya yote nina chukua fursa hii kukiri kwa dhati kwamba muda wote wa miaka mitatu na ushei wa uongozi wako………hujaingilia uamuzi wa mahakama kwa matendo wala kwa kauli, waliokutangulia waliwahi kuteleza na kuvunja mwiko huo. Lakini hatuwazungumzii hao na isitoshe, yaliopita si ndwele,” alisema Jaji Mkuu.

Aliongeza “hivyo ndugu zangu Majaji na Mahakimu, tumpongeze kwa kishindo Mheshimiwa Rais kwa kuwa muumini na kielelezo cha kuheshimu dhana ya mgawanyiko wa madaraka kwa vitendo na kauli,” alisisitiza.

Kuhusu Bunge, bila kujali uwapo wa Spika wa Bunge, Samuel Sitta katika hafla hiyo, alisema mhimili huo uliwahi kutaka uwe na madaraka ya kimahakama dhidi ya watu ambao wanazozana na Wabunge lakini wazo hilo halikufanikiwa ingawa kinyume cha utaratibu lilichukua kazi ya mahakama ya kusikiliza tatizo kati ya Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima na Reginald mengi ambaye si Mbunge.

Aidha pia alisema Spika wa Bunge, Sitta, katika kile alichokiita kughafilika aliwahi kutoa matamshi kuhusu sakata la mafuta ya petroli huko Morogoro baada ya amri ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji, Ewura ya kuvifunga vituo kadhaa vya mafuta ilipositishwa kwa muda na Mahakama ya Hakimu Mkazi.

No comments:

Post a Comment