“Nikamwita askari wangu nikamwambia Mwalimu Mkuu atoke, tukafunga mlango nikawaambia walimu kama watoto wanaochelewa mnawapa adhabu na mimi nawapa adhabu,” alisema Mnali kuthibitisha kucharazwa viboko vinne kila mmoja.
Walimu waliocharazwa ni Generosa Lwakatare, Ernestina Anatory, Jonesta Grenos, Hawa Ayubu, Rehema Baisi, Frieda Laurian, Avitus Leonald na Asirath Ndyamukama wa Katerero.
Wengine ni Amos Kamugisha, J.K. Zale, Bruno Francis, M. Mwesiga, Pulleti Rugemalila, Winfrida Kakurwa, Editha Bigilwa, Ester Mutashaba, Ludovic Bushongole, Gosbert William, Venance Philipo na Vedasto Munabi wa Kansenene.
Walimu wengine waliochapwa ni Imelda Lwegalulira, Coretha Ernest, Devotha Bushobe, Augustina Bampenja, Josephina Ndyamukama, Julius Katemana, Videlieth Yesse, Generoza Mulokozi, Sylvester Petro, Josiah Kamuhabwa na Concessa Rweyemamu wa Kanazi.
“Ni kweli tukio hilo limetokea … ni vyema DC na huyo Polisi wakapimwa afya kwa sababu hii si hali ya kawaida, kwani zipo taratibu za kinidhamu za kuchukua kwa watumishi,” alisema Naibu Waziri wa Elimu MWANTUMU Mahiza ambaye kitaaluma ni mwalimu.
Ama kweli huu ni ulevi wa madaraka uliopitiliza. Kwanza, nawashangaa hao walimu kukubali adhabu hii. Nadhani hawafahamu vizuri haki na stahili zao.
ReplyDeletePili,Nashangaa pia kwa nini huyu DC hajachukuliwa hatua. Mamlaka yake ya nidhamu ilitakiwa iwe imemwajibisha kabla hata vyombo vya habari havijapata taarifa.
Huu ni mfano mmojawapo wa viongozi kujitwalia madaraka wasiyokuwa nayo.
Je, wanafunzi wao watawaheshimu vipi walimu wao walidhalilishwa.
Walimu hawa wammepeleke mahakamani kwa kuwadhalilisha na kuwaletea maumivu.
Mdau
Faustine
http://drfaustine.blogspot.com/
Hii hawa bado wako kazini?, nadhani walitakiwa kufutwa kazi mara moja. Ama mpaka musikie wameua, anayehusika kuwachukulia hatua halioni hilo?, au mpaka naye pia aunganishwe nao?.Ila nawashauri waliofanyiwa hivyo waende mbele ya sheria.Mwisho msikubali kila kitu mkuu wa wilaya ni mtushi wa kawaida tu kama nyie msiwe waoga wa madaraka.jg.
ReplyDeleteMi namuunga mkono mia kwa mia huyo DC kwani hapa TZ nadhani hali imefikia hapo, tena ingekuwa amri yangu ningepitisha iwe sheria kila anayefanya kosa ni kiboko tu ndo adabu itarudi.
ReplyDeleteMambo mengi yanayofanyika nchini au kwenye asasi mbalimbali za serikali yanatia kinyaa na hasira sana mtu atekelezi wajibu wake ipasavyo ukiuliza sababu haijulikani. Yaani hapa kwanzanilitakiwa baada ya kuwatia hao mboko naye pia aitwe na mkuu wake wa mkoa hapate zake pia kisha mnyororo uendelee vivyo hivyo hadi juu kabisa, kwani ukiangalia kwa undani sana utaona matatizo ya wanafunzi kufeli si ya mwalimu pekee sana waweza kuta chanzo kikuu ni serikali yenyewe, so ka ni kuchapwa si walimu tu bali hadi watendaji wakuu wa serikali wanaoleta siasa katika mambo nyeti ka ELIMU.
INATIA UCHUNGU SANA, SERIKALI IFIKIRIE KUWEKA ADHABU YA VIBOKO KWA WOTE WANAOZEMBEA.
MDAU.