Pages

January 22, 2009

Ubishi mwingine!!! ati OBAMA hakusoma speech yake!!!!!!

Nimekuta ubishi paala fulani tena kwa watu naweza sema ni waelewa kiasi fulani maana wameenda shule na wengine wako katika fani, ati ile hotuba aliyotoa mara baada ya kuapishwa ati hakuwa akisoma popote ila ilikuwa yatoka kichwani tu!!!

Nilishangaa sana kusikia vile, lakini nikaona si vyema nikanyamaza nikaona nililete kwenu wadau, je kuna anayehamini kuwa BO alikuwa hasomi ile speech?

Nawaombeni nitumieni maoni yenu tafadhali ili tusaidie wale wasiojua ili angalau wapate mwanga.

14 comments:

  1. Anonymous5:58 PM GMT+3

    SASA HAPO MBISHI NANI KA SIO WEYE? WE ULIONA ANASOMA WAPI AU UMEADITHIWA TU?
    KILE KICHWA BWANA, ANAWEZA MWAGA SERA MASAA BILA KUSOMA KOKOTE AU UKUONA KAMPENI ZAKE NINI?
    ACHA KUWAPIGA FIX WATU BWANA.

    ReplyDelete
  2. Anonymous6:26 PM GMT+3

    Mh!! sitii neno mie maana nsijitie kujua kumbe!!!!

    leteni data au mnaojua mtujuze nasi jamani,
    asante mzee wa bongo pix kutuletea hii mada maana huku kwetu mbagala watu walitaka toana macho kwa ubushi huu.

    ReplyDelete
  3. Anonymous9:07 AM GMT+3

    Some people got nothing to do for sure, what kind of debate of this now, how can some one talk of such rubish? this is what we call simple mind people, whats wrong with you tanjanians? you bongo pix did'nt you see that speech? that guy is geniues bwana he need not to read such simple speech.
    STOP THE DEBATE AND GO BACK TO WORK GUYS.

    ReplyDelete
  4. Ok. Ukweli ni kwamba alikuwa akisoma kwa kutumia hizo ziitwazo TELEPROMPTER ambazo wazion ahapo pembeni mwake. Ni aina ya vifaa mabavyo hu-reflect maneno na yeye kuyasoma. Ila ni lazima uwe mzuri kwenye kuvitumia ili kuweza ku-deliver speech nzuri. Ni muundo mpya ama wa kisasa zaidi ya ule unaotumika kwenye kusoma taarifa za habari kwenye TV.
    Unaweza kuangalia aina na matumizi ya teleprompter kwa kubofya http://en.wikipedia.org/wiki/Teleprompter

    ReplyDelete
  5. Anonymous1:52 PM GMT+3

    KUNA KAKIBAO HAPO MBELE JAMANI ILE NDO SPEECH YENYEWE.

    ReplyDelete
  6. Asante Mzee wa Changamoto kwa ufafanuzi wako, pia na wadau wote kwa michango yenu.

    Nimepeta picha za Nyuma ya pazia nitaziweka ili kuondoa ubishi na hili sote tuelimike juu ya aina hii tekelinalotujia.

    ReplyDelete
  7. Anonymous1:53 PM GMT+3

    hakusoma na sio hiyo tu, hajawahi kusoma speech yoyote hadharani.

    hali hiyo imezua maswali mengi likiwemo kuna sababau gani ya kuchagua msaidizi kwa ajili ya kumuandikia speeches ambazo hasomi.

    lakini bado mapema kwahivyo kwahili tusimuhukumu, inawezekana ni utaratibu aliokuwa amejiweka awali ambao kadri atakavyoizowea white house, ndivyo atakavyoendelea kubadilika.

    thnx

    ReplyDelete
  8. Anonymous1:54 PM GMT+3

    umetusaidia wengi tu. mie sikuwa najua hiyo technology by no way haikufanana na hotuba ya papo kwa papo. Hii ni kama ya habari katika tv au?

    ReplyDelete
  9. Tafadhalini msiwe wajinga kiasi hicho hebu tafuteni la maana la kufanya sasa ikiwa hiyo hotuba kaisoma au haikusoma wewe itakusaidia nini?

    ReplyDelete
  10. jamani ehee!sikieni kama mtu una mapenzi na mtu!yasizidi mipaka!watu mnaexaggerate mambo mpaka watu tunaosoma tunasikia aibu!speech iliandaliwa for abt 2months yeye obby na director wa speech wa white house(kajana wa umri wa miaka 27) obama alikuwa anasoma what was already written!the use of telepromter can make the reader seem not to be reading as the device can enlarge the words hence easly seen by the reader.

    ReplyDelete
  11. JE WADAU BADO MNA MAWAZO TOFAUTI AU TUMEPETA PICHA KAMILI YA KAMA ALISOMA AU LA?

    TOA MAONI YAKO JINSI UONAVYO WEWE NA SI LAZIMA UWE SAWA NA MWINGINE AU UFATE TU MLADI HUYU KASEMA HIVI.

    KARIBUNI.

    ReplyDelete
  12. weye umekuwa mpemba mara hiii yahe HUYO OBAMA PAMOJA NA KUWA YEYE NI KICHWA KAMA JK WA BONGO LAKINI ALIKUWA ANASOMA HATA JK KWENYE MJENGO ALITUMIA TEKNOLOJIA HIYO PALE KATIKATI YA BONGO YAANI MJENGONI. HATA HIYO HUYU OB NAEE ALITUMIA KIFAA HICHO PALE MJENGONI KWAOOOOOOOOOOO

    ReplyDelete
  13. Anonymous2:08 AM GMT+3

    Haki sijaona watu washamba kama nyie, Speech zote za Nchi zilizo endelea zina andaliwa na kusomwa na hata coppy hutolewa kabla , hata JK alipo hutubia Bunge siku siku ya kwanza baada ya kumuapisha Lowassa , coppy ya speech ilikuwepo.
    Mnadhani ni enzi za Nyerere kila kitu kutoa Kichwani na kukalisha watu masaa kusikiliza story? , wenzenu wana enda na muda kila kitu lazima kiwe planed .

    Obama alisoma hutoba hata kwenye campagn zake zote alikua ana soma na sio yeye tuu maraisi wote na speech zote zinazo andaliwa huwa zina somwa , kwakupitia hicho kifaa , hata kwenye show kama hizo Awards ceremonies ukiona celebrity wana present Award huwa wana soma .
    JK pia siku hiziz ana soma kupitia hicho kifaa kwenye hotuba zake za mwisho wa mwezi.

    ReplyDelete
  14. Anonymous4:58 AM GMT+3

    Unajua ndiyo maana watu wengi wako brain-washed na Obama. Kwa taarifa yetu hata hizo hotuba zake zote pamoja na za kampeni alikuwa nasoma na hakuandika yeye kuna dogo anaitwa Jon Favreau ndiye anayemuandikia yeye kazi yake kusoma tu.

    ReplyDelete