Pages

January 2, 2009

Sikiliza Bibi Umeme!

Mabibi Umeme Badra Masoud (Msemaji Mkuu) na Evalder Munisi (Mhandisi Mkuu) wakionyesha jinsi watu wasiopenda maendeleo au wapenda kukaa kizani walivyujumu miundo mbinu ya shirika huku Pugu, Majohe.
Nyaya zenye ulefe wa mita zipatazo 3,0000 zimeibwa na hasara isiyopungua millioni nane, tanesco wameamua kusitisha kupeleka huduma hii huko kutokana na hujuma hii.
Hili ni eneo jipya kabisa lenye wakazi wapatao elfu na ushhee ambapo tanesco walijaribu kuwasogezea huduma hii muhimu kwa matarajio kuwa wangepata wateja wapya wapatao mia nane hivi, lakini hadi kufikia jana ni wateja wapatao 45 tu ndo walikuwa wameomba kuunganishiwa.

2 comments:

  1. Anonymous5:13 PM GMT+3

    Kazi ipo!:-(

    ReplyDelete
  2. Umasikini ni mbaya, lakini umasikini mbaya kuliko wote ni umasikini wa fikira njema!
    Walioiba nyaya za umeme ni masikini wa akili, hata kama ni umasikini wa mali na hali ya maisha kuwa ngumu, bado kuhujumu huduma muhimu kama umeme ni umasikini wa fikira njema!
    Kuwalipiza viongozi wasio waadilifu kwa kuwaadhibu wananchi wanaohitaji umeme si sawa. Ubaya haujengi.

    ReplyDelete