Habari hii inasikitisha sana, ya mtu kukamatwa, kufungiwa gazeti tando lako ambalo umekuwa ukilitumia kuwasiliana jamii, kufikisha ujumbe na kuelezea kile unadhani ni ukweli na kukabiliwa na kesi pengine kuadhibiwa kifo kwa kueleza hisia zako tu? Huyu bwana Hamoud Bin Saleh hatakuwa wa kwanza "KUIJUA KWELI" bali yawezekana kosa lake ni kutaka na wengine hasa nduguze wa Saudi waijue kweli hii pitia blog yake ya www.christforsaudi.blogspot.com ndilo limekuwa kosa. Wale tunaoperuzi vitabu vitakatifu kuna kimoja kinasema na nanukuu " NA WATAIJUA KWELI NA HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU" swali je kweli ni ipi? Mwalimu Nyerere alipata kusema kuwa hakuna vita ya kijinga kabisa kama vita ya kidini, kwasababu dini ni imani ambayo kwanza hukuzaliwa nayo na waweza kubadili kadiri ama kuama moja kwenda ingine wakti wowote kadri uonavyo yafaa au ushawishi wake, lakini si kabila kwani kama we ni mgogo, mhaya, mhehe NK hata ufanyeje uwezi kubadili hilo. WANABLOG MWASEMAJE KUHUSU HATUA HII YA SERIKALI YA SAUDI?
JE DUNIA HII TULIONAYO YA SAYANSI NA TEKELINALOTUJIA SHERIA KANDAMIZI KAMA HIZI ZINA NAFASI GANI BADO KATIKA DUNIA KIJIJI YETU HII?
asante, hili ni tatizo la kidini, mi nadhani serikali ya Saudia ingewapa watu uhuru wa kuabidu na kuwa huru na imani yao. Haijalishi ni dini gani. Injili bado inaendelea kuhubiriwa kila mahali hata wapinge vipi!
ReplyDeleteKama navyo chukia Waislamu wamsimamo mkali wanvyo anza kuingia western world na kutaka kuleta culture yao isiyo na haki za binaadamu, pia na dhani Mhusika hapo alitakiwa aheshimu culture za hao waarabu na kuzifuata kama zilivyo nadhani asinge pata tatizo lolote.
ReplyDelete