Pages

December 17, 2008

WAANDISHI WATUNUKIWA

Father Kidevu Mroki akipewa nishani
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Amiri Jeshi Mkuu, wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jakaya Kikwete amewatunukia nishani waandishi 12 wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, walioshiriki katika vita ya kumng’oa kiongozi muasi ndani ya visiwa vya Komoro, Kanali Mohamed Bakari. Akikabidhi nishani hizo, kwa niaba ya Rais kwenye viwanja vya Karimjee Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema taifa limethamini mchango wa wanahabari hao, waliokuwa wakiripoti katika mazingira magumu, dhidi ya vita hiyo. “kwa kutambua mchango wako, (mmoja mmoja) wa kuandika matukio kwenye uwanja wa mapambano, wa kukikomboa kisiwa cha Anjouan, yaliyofanyika bila kumwaga damu, kazi uliyoifanya katika mazingira magumu, mimi Rais nakutunukia nishani,” alitamka.

No comments:

Post a Comment