Pages

December 19, 2008

Hatutakwona tena Hery Makange.

Safari kuelekea Kibaha kwa Mazishi hapo kesho inaanza.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Abdalah Msika akitoa heshima za mwisho
Mjane Jane Makange akisali mbele ya jeneza.

Tangu pale nilipojuzwa juu ya msiba wa Mpiganaji Hery Makange na Father Kidevu sikutaka kukubali, ni akili ya kibinadamu, lakini hata pale nilipojaribu kuulizia kwa jamaa wa karibu na hasa zaidi baadhi ya wafanyakazi wenzake pale Chanel TEN bado sikutaka sadiki moja kwa moja, ndivyo tulivyoumbwa! Lakini zaidi hata pale nilipochukua jukumu la kuujulisha umma juu ya msiba huu kupitia blog hii bado akili yangu ilikuwa ikinituma kuwa si halisi bali ni ktk zile ndoto za jinamizi jitupatazo tuwapo usingizini.

Leo hii ninaposhuhudia Mpiganaji kalala sandukuni haamki tena! Nimwangaliapo mjane akilia japo akijitia nguvu na kukumbuka kuwa ndo kwanza wamemaliza "mwezi asali" au Honey Moon namwonea huruma sana na machozi kububujika bila kutaka na nadhani labda yeye ndo aonaye au adhaniaye kuwa hii ni moja ndoto mbaya kabisa na pengine anaomba azinduke na kumkuta Hery akiwa ubavuni mwake na kumuhakikishia kuwa hasiofu kitu bali ni ndoto tu!!

Lakini ahh! hivyo sivyo ilivyo bali haya yote ni halisi kabisa na wala si ndoto hata kidogo, Ni kweli kuwa Ndugu yetu, Rafiki yetu na mpendwa wetu Hery hatunaye tena, amelala usingizi mzito, ametutoka na ametangulia mbele za haki hatutamwona tena.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

1 comment: