"Hii sirikali ya awamu ya nne ni chiboko yaani hata miye nalala selo hati kwa kukosa tubilioni tunne tu??? walai siamini, hebu kachukue lile VX langu pale kwa Hoseah kijana".
kwa kweli siami macho yangu au naota vile?
MAWAZIRI wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona, wamelala rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana baada ya kushitakiwa kwa kosa la kuisababishia hasara serikali ya Sh bilioni 11.7. Washitakiwa hao ambao walipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana saa 5:35 asubuhi, walishindwa kutimiza sharti la kila mmoja kuweka Sh bilioni 3.9 mahakamani. Walikana mashitaka yao 13. Wote wanatuhumiwa kutumia vibaya madaraka yao ya uwaziri hivyo kuipendelea Kampuni ya Alex Stewart (Assayers) ya Uingereza kwa kuipa misamaha ya kodi.
http://www.dailynews.habarileo-tsn.com/
3 comments:
hii ni kali kweli mdau, siamini masikio yangu ka watu kama hawa wanaweza kweli kushtakiwa au kulala selo duuh
ila jamaa hawa wanalala kweli keko au danganya toto? naomba mdau chunguza ilo kisha tujulishe tuaaminia blogu yako mzee.
Mdau Zenji.
HA TI MA YE
SIO CHANGA LA ..............WADAU???
Post a Comment