Pages

November 27, 2008

TAHLISO WAIBUKA...

Tanzania Higher Learning Institutions Students Organization (TAHLISO) Chairman Christopher Ngubiagai (C) speaks during press brief. Others L – R Manyama George (Commisioner from SAUT), Iman Batenzi (Senator- Mzumbe), Nicholas Mtindya (Sectetary General – Tumaini), Pangani Peter (Treasury - TIA), Joram Malimi (Senator- UDOM) and Kapinga Angelus Senator – Ruaha).

UMOJA wa wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO)umesema unatambua na kukubaliana na madai ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu lakini hawaamini kama migomo ndiyo suluhisho la madai hayo.

Aidha ,wamesema sera ya uchangiaji wa elimu ya juu haiwezi kuepukika ila kinachotakiwa ni kufanya marekebisho katika kutambua mtoto wa tajiri na masikini mara wanapotaka kupewa mikopo.

Akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu msimamo wa umoja huo kuhusiana na migomo katika vyuo vya elimu ya juu nchini,jijini Dar es salaam jana,Mwenyekiti wa umoja huo Christopher Ngubiagai alisema Wanafunzi hao wanatakiwa utumia busara ,hekima ,maarifa na ujuzi wa kielimu walioupata na wanaoendelea kuupata katika kufanya maamuzi sahihi kwa njia ya majadiliano.

“TAHLISO inatambua na kukubaliana kuwa,madai yote ambayo wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wanadai ni sahihi na ni halali kabisa na ndio maana iliyaainisha na kuyawasilisha serikalini Tangu mwezi Julai mwaka huu lakini haitambui migomo iliyofanyika na baadhi ya vyuo vichache vya umma”Alisema

Naye ,Katibu Mkuu wa Umoja huo Nicholas Mtindya alisema , madai yote ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu tayari yamepitiwa katika mchakato wa mazungumzo ambao uliishafanyika kati ya TAHLISO na serikali kupitia Waziri wa Elimu Oktoba 23,mwaka huu.

1 comment:

  1. Kaka Ben,
    Asante kwa picha za matukio mbalimbali na habari mpya unazotupa kila mara.
    Kazi njema kaka na daima pamoja!

    ReplyDelete