MAHAKIMU wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam ambako kesi za ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinasikilizwa, wamehofia usalama wao; hali iliyowalazimu kuomba kupatiwa ulinzi wa polisi.
Mahakimu hao wanadai wamepewa dhamana ya kuendesha kesi hizo kubwa wakati usalama wao ni mdogo kutokana na kutokuwa na usafiri, hali inayowalazimu wakimaliza kuendesha kesi hizo wapande daladala.
No comments:
Post a Comment